Haondoki Ng'o: Juventus


 
Nyota wa Ufaransa Paul Pogba anawindwa na miamba wa ligi kuu Uingereza Manchester United

Na Dan Ogega

Manchester United iko tayari kumnunua Paul Pogba kutoka Juventus lakini usajili huo hauko karibu kukamilika. Uvumu kuhusu United kupeleka toleo la pauni laki moja umekuwa ukisambaa katika vyombo vya habari nchini Uingereza, lakini sasa Juventus imethibitsha kuwa haijapokea ofa yoyote kutoka kwa klabu hiyo inayoshiriki ligi Uingereza.

Kwa sasa Pogba, mwenye umri wa miaka 23 anatilia maanani maandalizi ya mchuano wa fainali dhidi ya taifa la Ureno ambao unagarazwa Jumapili tarehe 10.

Hata hivyo Juventus haijafa moyo kumshawishi Pogba kusalia nao katika siku za usoni huku mkurugenzi mkuu wa klabu hiyo akisema kuwa watafanya kila wawezalo ili kuhakikisha kuwa mfaransa huyo anasalia kiwarani Turin. 

Habari zimezagaa nchini Uhispania kuwa mfaransa huyo anapendelea kujiunga na mabungwa wa klabu bingwa barani Ulaya Real Madrid.

Pogba aliwakilisha Manchester United, kwa miaka miwili kabla ya kuhamia Italia mnamo mwaka  2012
Share on Google Plus

Kuhusu Unknown

Michezo Kenya Tunapenda Spoti

0 comments:

Post a Comment