Klabu inayoshiriki
ligi kuu Ujerumani Wolfsburg imetengaza kuwa kiungo wake Julian Draxler
hataruhusiwa kuondoka Mercedes Benz Arena msimu huu.
Habari hizi
bila shaka ni bonge la kigongo kwa klabu ya ligi kuu Uingereza Arsenal ambayo
inasemekana kuwa ilikuwa tayari kupeleka ombi la kumnyakuwa kiungo huyo.
Wolfsburg
ilimaliza nje ya timu zinazoshiriki ligi kuu mabingwa barani ulaya katika ligi
ya Ujerumani Bundesliga na kisha mkurugnzi wake mkuu Klaus Allofs akafichua
kuwa klabu hiyo ilikuwa radhi kumwuza kiungo huyo ambaye zamani alisakatia
Shalke 04. Kwa sasa Draxler amesalia na muda wa miaka minne katika kandarasi
yake huku Wolfsburg ikiitisha kitita cha pauni milioni 55 kutoka kwa klabu
yoyote inayopania kumsajili kabla ya mkataba wake kutamatika.
Sasa Allofs
amegeuka kinyonga na kusema kuwa sasa Julian hauzwi tena.
"Julian
haondoki hapa hata kwa jinsi gani. Nina uhakika kuhusu hilo kwa asilimia 100,"
Allofs alinukuliwa na kituo cha habari cha Sport1.
"Hakuna
mjadala kuhusu hilo."
Arsenal iko
katika hali ya hati hati ya kumtafuta msaidizi wa Olivier Giroud katika safu ya
ushambulizi baada ya kuzikosa huduma za Jamie Vardy kutoka Leicester.
Kabla ya
kutua Wolfsburg Draxler alihusishwa pakubwa na kuhamia Arsena mnamo mwaka 2013 lakini
ikamsajili Mesut Ozil badala yake.

0 comments:
Post a Comment