Mshambulizi
mpya wa klabu iliyomalia katika nafasi ya pili katika ligi kuu ya mpira wa
vikapu Marekani New Golden State Warriors Kevin Duran amesema kuwa uhusiano
wake na mchezaji mwenza wa zamani wa klabu ya Oklahoma City Thunder Russell
Westbrook hautasalia tena kuwa kama zamani na itambidi kuzoea mazingira hayo.
Akizungumza
na Shirika la habari la Sina Sports Durant amesema kuwa alizungumza naye Westbrook
kabla ya kutia saini kandarasi ya miaka miwili na Warriors. Sasa itambidi
Durant kumenyana na mawiji wengine katika kikosi kilichosheheni mastaa wengine akiwemo
mchezaji bora NBA msimu uliopita Steph Curry, Klay Thompson na Dreaymond Green
hili kujihakikishia nafasi katika kikosi cha kwanza.
Nilizungumza
naye na nikamwelezea mawazo yangu.’’
"Kijumla
ni kwamba mahusiano yangu naye hayatasalia kama zamani. Nilizungumza naye na ni
matumaini yangu kuwa ataheshimu maamuzi niliyoyafanya.’’
Pia Durant
anasisitiza kuwa jambo kuhusu Warriors kubandikwa jina la maadui halimbabaishi
kabisa.
"Kwangu
itaniwia vigumu katika hatua za mwanzo kwani sijazoea kumulikwa na umati mkubwa
kama sasa. Lakini natumai kuwa nitazoea. Watu wengi hawanipendi hivi sasa na
bila shaka wana sababu zao. Naamini kuwa jukumu langu ni kutekeleza majukumu
yanayoambatana na wajibu wangu kwa sababu siwezi kufurahisha kila mtu.
Sasa
Kevin Durant anaamini kuwa jukumu lake kuu litakuwa kuisaidia Golden State
Warriors katika harakati za kuwinda taji la ligi ambalo walilipoteza baada ya
kupepetwa na Cleveland Cavaliers katika fainali kuu msimu uliopita.

0 comments:
Post a Comment