Time Peake akiwa angani
Eliud Kipchoge aliongoza washiriki takriban elfu 38,000 jana Jumapili katika mbio za London Marathon huku mpinzani mmoja akishiriki shindano hilo akiwa maili 200 juu ya sayari ya dunia.
Mwanasayansi muingereza Tim Peake alikamilisha mbio hizo za kilomita 42 au maili 26.2 akiwa katika kituo wanasayansi cha International Space Station kwa muda wa 3:35.21 ,jambo ambalo ni la kwanza kutokea katika historia ya riadha. Haya ni kwa mujibu wa shirika la anga la bara Uropa ESA.
"Wakati tu unaacha kukimbia misuli yako huwa imetulia kabisa na pia kupona kutokana na maumivu huchukua muda mrefu sana."
Eliud Kipchoge akisherekea ushindi LondonKatika mbio hizo Eliud Kipchoge alilitetea taji la wanaume ikiwa ni sekunde nyuma ya rekodi ya dunia baada ya kukata utepe mbele ya kasri ya Buckingham kwa muda wa 2:03:05. Mkenya mwingine Jemima Sumgong alishinda taji la wanawake baada ya kukata utepe baada ya 2:22:05.
0 comments:
Post a Comment