Kaimu meneja wa Manchester United Ryan Giggs atagura
klabu hiyo ikiwa Jose Mourinho atateuliwa kufundisha klabu hiyo msimu ujao. Wakati
huo huo idadi ya tiketi za msimu zinazonunuliwa imeongezeka licha ya klabu hiyo
kusajili matokeo duni msimu huu.
Meneja wa klabu ya ligi kuu Uholanzi Ajax Amsterdam Frank de Boer ameonyesha nia
ya kujiunga na miamba wa ligi kuu Uingereza Everton msimu kesho. Hii ni kwa
mujibu wa wakala wake. Haya yanajiri huku shinikizo za kumuondoa meneja wa sasa
Roberto Martinez zikizidi kushika kasi. Robbie savage pia anahisi kuwa mkufunzi
wa Newcastle Rafa Benitez anafaa kuridhi mikoba ya Martinez huko Liverpool.
Mchezaji bora msimu nchini Uingerza Riyad Mahrez
aliye na umri wa miaka 25 atakataa ombi la pauni milioni 40 la klabu za
Arsenal, Barcelona na Paris St- Germain ili
kusalia na mabingwa wa ligi kuu Leicester City.
Leicester pia wanajiandaa kumnunua mshambulizi wa Pescara
Gianluca Lapadula, ambaye amefunga mabao 24 msimu huu katika ligi ya daraja la
pili Italia Serie B.
Wakati huo huo meneja msaidizi wa Leicester Steve Walsh ambaye pia ni mkuu wa
kitengo cha ununuzi wa wachezaji, ametia saini mkataba mpya ili kuendelea
kuhudumia mabingwa hao wapya wa ligi kuu Uingereza.
Wachezaji Leicester City wakisherehekea ushindi wa ligi kuu
Maelfu ya mashabiki wa
Manchester City hawakuhudhuria hotuba ya mwisho ya meneja wa klabu hiyo anayeondoka
Manuel Pellegrini baada ya kusajili sare ya 2-2, hali ambayo huenda ikawafanya
City kukosa kumaliza ndani ya nne bora msimu huu.
Mmiliki wa Manchester City walimkabidhi Sheikh
Mansour alimkabidhi Manuel Pellegrini mchr halisi wa LS Lowry kama zawadi ya kuondoka kabla ya
kumpisha Pep Guardiola msimu kesho.
Aitha Pellegrini
aliye na umri wa miaka 62 anasema kuwa klabu hiyo imeimarika chini ya uongozi
wake licha ya uwezekano wao wa kushiriki Champions Lague msimu ujao kukumbwa na
hati hati.
Kiranja wa Manchester
City Vincent Kompany aliye na umri wa 30
atakuwa nje ya dimba hadi msimu ujao kwa sababu ya jeraha.
Chelsea itarejea Everton na ofa ya pauni milioni 40
kwa ajili ya kumnyakua mlinzi John Stones aliye na umri wa miaka 21. Everton
wanasisitiza kuwa lazima Chelsea watoe ofa ya pauni milioni.
Klabu hiyo inayochezea
michuano yake ya nyumbani katika kiwara cha Stamford Bridge imeanza kukumbwa na
masaibu baada ya meneja wake mpya Antonio Conte kukatazwa kuambatana na
wasaidizi wake wawili.
Chelsea wanapania kuziba pengo litakaloachwa na John Terry kwa kumsajili John Stones.
Kiranja wa muda mrefu wa klabu hiyo John Terry anatarajiwa kuondoka mwisho wa msimu huu.






0 comments:
Post a Comment