Nipo Tena Sana: Payet
Dimitri Payet akisherehekea ushindi wa klabu yake ya Westham msimu uliopita.
Na Dan Ogega
Klabu
inayoshirki ligi kuu nchini Uingereza Westham United imepiwa jeki katika
harakati zake za za kufanya vyema msimu ujao baada ya mchezaji wake mbunifu
mfaransa Dimitri Payet kukariri kuwa kamwe hatahamia kwingine katika msimu wa
joto. Hili linajiri baada ya uvumi kuenea kuwa mabingwa wa klabu bingwa barani
Ulaya msimu jana Real Madrid walikuwa tayari kupeleka toleo kubwa kwa ajili ya
kumnasa mchezaji huyo.
Payet
alifana sana katika dimba la taifa bingwa barani Ulaya lililoandaliwa nchini
mwao Ufaransa hali ambayo ilikolesha wino tetesi kuwa huenda miamba wa soka
barani humo kama Real Madrid, Juventus na Man Unites wangefukuzia saini yake.
Hapo
awali mmiliki mwenza wa timu hiyo David Gold alikuwa ameweka bayana kuwa klabu
yoyote ambayo ilikuwa na nia ya kumnasa mfaransa hiyo lazina ingetengana na
kitita kisichopungua pauni milioni 50.
Lakini licha
ya tumbojoto hili wafuasi wa nyundo wana kila sababu ya kutabasamu baada Payet
kudhibitisha kuwa kamwe hatong’atuka klabuni humo na yuko tayari kuwakilisha Westaham
katika kampeini yake ya kwanza katika uwanja wake mpya wa Olympic jijini London
msimu kesho.
“Nina
habari kuhusu klabu kubwa kutaka huduma zangu lakini kwangu hiyo ni ishara ya
watu kutambua kazi nzuri ninayoifanya," alisema Payet.
"Kwangu
jambo la msingi ni kuwa ninaienda sana West Ham. Msimu jana tulikuwa na
mafanikio makubwa na natumai mambo yatakuwa mazuri msimu kesho kwa sababu
tutachezea mechi zetu za nyumbani katika uwanja mpya.
“Nina
uhakika asilimia 100 kuwa siendi popote, nina mapenzi ya dhati kwa klabu hii na
huu ndio ujumbe wangu kwa wananyundo wote.”
Aidha hii
ndio kauli ya mmiliki mwenza wa klabu hiyo Gold ambaye hapo kabla alikuwa amehapa
kufanya kila jambo hili kuhakikisha kuwa mchezaji huyo anasalia na wananyundo
msimu kesho

0 comments:
Post a Comment