Man Utd Kuvunja Benki kwa Ajili Bale

 

  Manchester United in imani kuwa itamnyakua Gareth Bale kutoka Real Madrid kwa bei ambayo huenda ikavunja rekodi ya dunia katika soko la wachezaji ambayo inakisiwa kwa pauni milioni 94.6
Paris St-Germain inatathmini kuilipa Barcelona takriban pauni milioni 153 ili kumnyakuwa Neymar Santos.

  Mshambulizi wa miamba wa Italia Juventus Alvaro Morata atakataa nafasi ya kujiunga na Manchester United ikiwa Zlatan Ibrahimovic atawasili Old Trafford.

  Uhamisho wa Ibrahimovic kwenda Old Trafford huenda usifanyike kulingana na meneja wa timu ya taifa la Sweden Erik Hamren ambaye anasema kuwa huenda straika huyo asicheze ligi kuu Uingereza msimu ujao.

  Manchester City iko tayari kumsajili kiungo wa klabu ya Athletic Bilbao Aymeric   mkataba wa miaka sita hasa baada ya kumuachilia Muajentina Martin Demichelis.

Straika wa Ubelgiji na klabu ya Marseille Michy Batshuayi, 22, anataka mshahara wa pauni laki moja ikiwa atajiunga na Tottenham Hotspur.
Share on Google Plus

Kuhusu Unknown

Michezo Kenya Tunapenda Spoti

0 comments:

Post a Comment