Old Trafford Siji Ng'o: Zlatan


Manchester United ina imani kuwa Zlatan Ibrahimovic, 34, atawasili Old Trafford licha ya wakala wake kusema kuwa huenda akajiunga na klabu nyingine. 

Kiungo Yaya Toure, 33, anajiandaa kumwambia meneja mpya wa Man City Pep Guardiola kuwa anataka kusalia Etihad baada ya kukataa kuhamia ligi ya China
Arsenal inaogopa kuwa kiungo wake Mesut Ozil huenda akajiunga na Bayern Munich baada ya kukataa kusaini mkataba mpya na klabu hiyo.
Liverpool itahitajika kukohoa kitita cha pauni milioni 45 ikiwa watamsajili beki mbrazil Aleix Vidal, 26, kutoka Barcelona. Vidal hatapewa nafasi ya kuziba pengo la Dani Alves, 33, atayehamia Juventus.
Beki wa Arsenal Hector Bellerin anasema kuwa nanavutiwa na hatua ya klabu ya Barcelona kumnyemelea. Barca inataka kuziba mwanya utakaoachwa na Dani Alves ambaye atahamia Turin.
Wakala wa straika wa Bayern Munich Robert Lewandowski anefichua kuwa huenda Mpolandi huyo akahamia Real Madrid baada ya kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Los Blancos.
Antonio Conte hataki kuiuzia Manchester United kiungo wake Willian, 27, kwa sababu anahisi kuwa mbrazil huyo ni kiungo muhimu kwa klabu hiyo.

Share on Google Plus

Kuhusu Unknown

Michezo Kenya Tunapenda Spoti

0 comments:

Post a Comment