Na Dan Ogega
Mchezaji wa timu ya taifa ya Cameroon Patrick Ekeng
amekuwa wa hivi punde kupoteza maisha yake uwanjani akicheza baada ya kuzimia,
jambo ambalo limeibua mawimbi ya hofu kuhusu usalama wa afya za wachezaji
kutokana na mazoezi wanayoyafanya. Mwingine aliyeponea kifo kwa tundu la
sindano ni kiungo wa zamani wa klabu ya Bolton Wanderers Fabrice Muamba, ambaye
alizimia kwa muda wa masaa 72 kabla ya kuudiwa na fahamu, huku daktari ake
akimshauri kuachana na uchezaji baada ya kupona kabisa.
Fabrice Mwamba alilazimika kutundika daluga zake baada ya kuzimia uwanjani
Takwimu zinapendekeza kuwa angalau wachezaji sita
wamepoteza maisha yao kwa muda wa miaka mitatu iliyopita kutokana na ugonjwa wa
mshtuko wa moyo. Pia ni nadra kuwa mwaka mmoja kupita bila ya kisa cha
mwanariadha wa masafa marefu kuripotiwa kuaga dunia kutokana na maradhi ya yaya
haya.
Habari kama hizi bila
shaka hututia hofu kwa kuwa huashiria mwisho wa maisha ya mwanaspoti ambaye alikuwa
na maazimio makubwa ya kuleta ufanisi katika taifa lake na pia familia. Jambo
lililo bayana ni kuwa sio wachezaji profeshenali pekee ambao hukumbwa na misiba
sampuli hii bali pia wale ambao wanajikuza kwa namna fulani. Ropiti za
afya zinasema kuwa mwanaspoti yeyote anayefanya mazoezi mazito kuliko kimo
chake yuko hatarini kuadhirika na maradhi ya mshtuko wa moyo.
“Wengi wa wanamichezo hasa wa kiume hufariki
kutokana na vyanzo vinavyojulikana na kila mtu,’’ anashauri Eric Larose ambaye ni
daktari wa moyo na mapafu katika hospitali ya Quebec nchini Canada.
Anazidi kuelezea kuwa idadi kubwa ya visa hivi ingeepukwa iwapo waathiriwa wangefahamu hatari na ishara za maradhi ya mshtuko
wa moyo.
Daktari mwingine Chris Woollam wa mbio za Mississauga
Marathon na Toronto Marathon anahoji kuwa vifo vinavyotokea katika mbio za
masafa marefu ni vya ajali tu, ingawa uwezekano wavyo kutokea ni wa chini mno
kwa waandalizi wa mashindano hayo kuweka mikakati ya kuwakagua wanariadha husika.
Ripoti ya utafiti iliyochapishwa katika jarida la matibabu la New
England Makala a mwezi Januari ilibainisha kuwa kati ya wanariadha
takriban milioni 10.9 walioshiriki mashindano mbali mbali ya riadha katika yam
waka 2000 na 2010, 59 walikuwa wanaugua maradhi hayo, hii ikiwa ni asilimia 0.54
ya washiriki wote.
Mmoja kati wa wanamichezo waliofikwa na mauti wakiwa nyugani
Asilimia kubwa iliwajumuisha wanaume maradhi ya mshipa ya
moyo ikiunga sehemu kubwa ya visa hivyo.
Pia hakuna uwezekano wa vifo vya ghafla kutokea
miongoni mwa wanariadha ikilinganishwa na idadi kamili ya watu.
“Kwa sababu
hii hakuna vigezo vilivyowekwa ili kuwakagua
wanariadha kabla ya mbio. Hali hii huwaachia jukumu la zito na kung’amua ikiwa
wako salama kukimbia au la.''…itaendelea…



0 comments:
Post a Comment