
Matumaini ya Arsenal kumnyakua Jamie Vardy kutoka Leicester City huenda yamezimika ghafla baada ya mchezaji huyo kukataa kufanya vipimo vya afya. Haya ni kulingana na madai ya sogora wa klabu ya Arsenal Ray Parlour ambaye alikuwa katika uwanja wa mazoezi wa klabu ya Arsenal Colney jijini London.
“Ni bayana kwamba uhamisho huu huenda usifanyike kwa sasa.
“Jana nilikuwa Colney na kulikuwa na ishara kuwa Vrady angekubali kutia saini kandarasi, kwa sababu wapiga picha walikuwa wameitwa ili kunasa matukio.
“Lakini huenda Vardy amegeuza uamuzi wake kuhusu hili.”
Katika siku za nyuma mkewe bi Rebekah alinukuliwa akiwakaripia mashabiki wa Leicester waliokuwa wakipinga Vardy kuhamia London.
Kwa sasa Vardy yuko na kikosi cha timu ya taifa la Uingereza katika michuano ya taifa bingwa barani Ulaya nchini Ufaransa.
0 comments:
Post a Comment