Je FKF Ilikuwa na Dosari Katika Maamuzi Yake?


                                                                                                                        Picha Ghettoradio    

    Na Dan Ogega
     Kushushwa daraja kwa klabu ya Shabana siku chache tu baada ya uongozi mpya wa shirikisho la soka nchini FKF kuingia ofisini, kulimushtua kila mshikadau katika soka ya Kenya. Hii ni kwa sababu klabu hiyo ilimaliza katika nafasi ya 10 msimu uliopita katika ligi kuu ya FKF jambo lililopelekea uongozi wa klabu hiyo kupitia katibu wake Peter Omwando, kukata rufaa kwa jopo la utatuzi wa mizozo ya masuala ya michezo. Aitha jopo hilo liliamua kuwa mazingira ya kushushwa kwa klabu hiyo yalikuwa ya utata na namo tarehe 19 mwezi Aprili likaamua kuwa klabu hiyo irudishwe mara moja kushiriki mechi za ligi ya dara la pili. Ni bayana kuwa haya ni kinyume cha matarajio ya uongozi wa FKF.
   Shabana hawakua timu pekee iliyosombwa na dhoruba la kushushwa daraja.  Klabu ya Hema moja FC inayoshiriki  ubingwa wa divisheni ya kwanza katika Zone B 2 iliyokuwa imeteremshwa daraja licha ya kumaliza katika nafasi ya sita ilirejeshwa pia baada ya maamuzi la jopo hilo
   Aitha vyuma vya vilabu vya Busia United na Lubinu Rangers bado havijaauniwa huku vikiendelea kusistiza kuwa hakuna sababu tosha za kushushwa kwao. Kulingana na katibu Jackson Makokha klabu ya Lubinu Rangers ilimaliza kileleni mwa divisheni ya keanza Zone B1 lakini wakanyimwa fursa ya kushiriki ligi kuu divisheni ya kwanza. Busia United nayo walimaliza wa nne lakini wakashushwa daraja badala ya kupandishwa ngazi.
   Sasa viongoz wa vilabu hivyo wamepanga kuwasilisha rufaa katika jopo hilo ili kutafuta haki. Maamuzi kam haya yatazidi kupaka tope nia ya uongozi wa FKF ikiwa jopo hilo litazidi kupata makosa katika maamuzi yake.
Share on Google Plus

Kuhusu Unknown

Michezo Kenya Tunapenda Spoti

0 comments:

Post a Comment