Kiranja wa zamani wa Kodivaa Didier Drogba. Picha Getty Images
Na Dan Ogega
Ni kawaida siku hizi kuwa mashabiki wengi wa
kiafrika wanaweza kutaja majina kamili ya wachezaji wa ligi kuu za Ulaya na kuelezea kwa undani kuhusu
taaluma zao. Lakini dhubutu kuwapa changamoto ya kutaja kikosi cha kwanza cha
timu ya taifa au klabu yoyote ya mtaani. Noma. Wengi watababaika na kusema
hawana ufahamu au ukibahatika watataja majina mawili au matatu huku pia wakichemsha
kuhusu habari za kina kuhusu wachezaji hawa.
Wamiliki wa
vilabu, mashirikisho yanayodhibiti soka na wizara za michezo kote barani
Afrika wote wanafahamu kuhusu kudidimia kwa ufuasi wa soka ya nyumbani, hali
inayochangiwa na mvuto wa ligi kuu mbali mbali barani Ulaya kama English
Premier League, La Liga, Bundesliga, Serie A na French Ligue 1.
Kwa bahati mbaya mifumo iliyobuniwa ya kutanganza
soka ya kiafrika na kuvutia mashabiki ambao hutumia muda mwingi kutazama
runinga na kufuatilia ligi zilizo mbali na makazi yao bado haijazaa matunda
yaliyotarajiwa. Mambo matano yafuatayo yamechangia hali hii.
Idadi ndogo ya mashabiki wakati wa michuano
Katika siku za wikendi na wakati wowote kunapochezwa ligi za Ulaya mashabiki ambao zamani walikuwa wakijitokea nyugani kushabikia klabu zao huwa wanatazama runinga ili wajue timu zao maarufu zinafanyaje, huku wakipuuza timu zao za mitaani. Badala ya kutumia kiasi kidogo cha pesa kuhudhuria michuano ya nyumbani, mashabiki wengi huona ni heri kununua kinywaji na kujumuika na marafiki wakifuatilia hali ya Wilshere, Diego Costa, Martial au Aguero.
Hali hii unavipokonya kipato cha kuuza tiketi vilabu vya mitaani na kuzidi
kuvifilisha. Ni bayana kuwa mashabiki hutokea tu wakati wa michuani
inayohusisha vilabu vyenye uhasama almaarufu derby au fainali.
Ukosefu wa muda wa kutosha katika vyombo vya habari.
Kwa sasa ligi za kiafrika zimekosa udhamini wa maana kutokana na uchache wa mashabiki wanaozifuatilia.
Wakurugenzi wa kampuni mbali mbali wanajitolea kufadhili ligi ambazo ziko na ufuasi mkubwa, hali ambayo huziweka pabaya zile zilizo na mashabiki wachache.
Ligi nyingi barani hazina namna ya kupeperusha
michuano yao kutokana na ukosefu wa wadhamini. Nyingi hutegemea michuanO ya
awamu za mwisho kama fainali ili kuvutia mashabiki wengi.
Wachezaji hutamani ligi za majuu.
Ligi kuu Uingereza ni baadhi ya vivutio kwa wachezaji wa kiafrika. Picha Sportslogos.netNi ndoto ya kila mchezaji kujiunga na ligi kuu za Ulaya na kuhepa hali duni ya miundo msingi inayokidhiri nyumbani mwao. Tabia hizi huwapelekea kuparamia nafasi za kujiunga na klabu yoyote ile inayoshiriki ligi hizi. Ni wachache mno huamua kusalia nyumbani kuwaburudisha mashabiki kwa kipato duni. Nani anaweza dhubutu kulaumu uongozi kwa kulipa mapeni machache wakali rasilimali hazipo?
Ufadhili Haupo
Kampuni nyingi za kimataifa hazina nia ya kununua klabu za kiafrika kama wangefanya kule ulaya Asia au Amerika kwa sababu ligi hizi hazina uwezo wa kuzalisha pesa nyingi.
Klabu nyingi husumbuka kupata
mikopo kutoka kwa benki ili ziimarishe miundo msingi au kununua wachezaji kwa
sababu hazina uwezo wa kulipa hiyo mikopo na riba inayoamatana. Timu hizi hutegemea msaada
wa serikali na kipato kidogo cha kuuza wachezaji ili kufanikisha maazimio yao.
Ligi hazijapewa kipaumbele na wahusika wenyewe.
Ni kawaida kuwa taswira kamili ya profeshenali
katika soka ni kucheza EPL au La Liga. Baada
ya kupata hela za mishahara, wao ndo hupewa nafasi katika jamii hali
inawapelekea kuchukua soka ya nyumbani na kutamani kupata mwanya na
kutoroka nyumbani.





0 comments:
Post a Comment