
Granit Xhaka atajiunga na Arsenal kwa kima cha pauni milioni 33
Na Dan Ogega
Manchester United itamteua Jose Mourinho kuwa meneja mpya baada ya pambano la fainali ya kombe la FA dhidi ya Crystal Palace katika uwanja wa kitaifa wa Wembley.
Straika wa Arsenal Alexis Sanchez, mlinzi wa Everton John Stones, na beki wa Tottenham Danny Rose ni miongoni mwa wachezaji wanaosakwa na meneja mpya wa Manchester City manager Pep Guardiola
Guardiola pia aanatumaini kumsajili kiungo wa Borussia Dortmund Ilkay Gundogan ambase alifanyiwa upasuaji wa goti.
Baba wa nyota wa Barcelona na timu ya taifa ya Brazil Neymar amedhibitisha kuwa Manchester United ilipeana toleo la pauni milioni 145 ili kusajili.
Leicester City inapania kunyakua winga wa Arsenal Theo Walcott, lakini muingereza huyoanataka kusalia jijini London.
Mauricio Pochettino anajiandaa kumwuza Son Heung-Minikiwa ni chini ya mwaka mmoja tangu raia huyo wa Korea Kusini kujiunga na Tottenham akitokea Bayer Leverkusen kwa kima cha pauni milioni 22, Pia yuko tayari kusikiliza ofa kwa wachezaji Nabil Bentaleb na Ryan Mason.
Arsenal itamshawishi straika wa Juventus Alvaro Morata na kandarasi ya miaka mitano na mshahara wa pauni elfu 155,000 kwa wiki, ili kuupiku upinzani kutoka kwa miamba wa London Chelsea.
Chelsea wanatumaini kumnyakua kungo mkabaji wa AS Roma Radja Nainggolan, licha ya mswizi huyo kuweka bayana yake ya kupenda kusalia na klabu hiyoya ligi kuu Italia
Everton wanataka kitita cha pauni milioni 23 kwa mchezaji wake Ramiro Funes Mori kufuatia klabu ya Lazio kumtaka kinda huyo.
Meneja moya wa Chelsea Antonio Conte ameanzisha mzungumzo na klabu ya Everton ili kusajili wachezaji wao wawili John Stones na Romelu.
Mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Antoine Griezmann atatia saini kandarasi mpya na miamba wa ligi kuu Uhispania Atletico Madrid ili kusalia nao kwa muda mrefu licha Manchester United kumnyemelea.
Huenda Moussa Sissoko, 26, akajiunga na Arsenal akitokea kuwa mchezaji wa kwanza kugura Newcastle
0 comments:
Post a Comment