Arsenal Kutesa Msimu Kesho




 
Wachezaji wa Arsenal wakisherehekea ushindi wa komBe la FA. Wenger anatathmini vyenye atawapiku wapinzani msimu ujao. Picha The Mirror. 
    Na Dan Ogega
Arsenal itamsajili kiungo wa Borussia Monchengladbach Grani Xhaka katika majira ya joto katika hatua za mwanzo za kujifua wakijitayarisha kwa msimu kesho huku David Ospina akitarajiwa kugura uwanja wa Emirates na kutinga Galatasaray. Ifuatayo ni tathmini ya jinsi Arsenali watajitanzua kutoka kwa masaibu yao msimu ujao.

The gunners walikosa taji la ligi kuu nchini Uingereza kwa tofauti ya alama kumi, lakini walifikia upeo mpya baada ya kumaliza katika nafasi ya pili katika kipindi cha muongo mmoja. Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ni mwingi wa furaha baada ya kunawiri katika msimamo wa ligi kuu lakini anajua kuwa wafuasi wa klabu hiyo hawajaridhika na ukosefu wa taji la ligi kuu kwa zaidi ya muongo mmoja.

Klabu hiyo ingeipiku Leicester City kama wangefunga nafasi zaidi ya 146 zilizobuniwa na kiungo mjerumani Mesut Ozil, hii ikiwa ni idadi kubwa zaidi katika ligi kuu ya premia nchini Uingereza tangu msimu wa mwaka 2003-04. Hakuna ubishi kuwa straika  Olivier Giroud ni mshambulizi matata lakini Arsenal haina budi ila umsajili mshambulizi wa hadhi ya juu atakayempa upinzani anaohitajika ili kuimarisha kampeini ya kusaka taji la ubingwa. 
 
Mesut Ozil alikuwa mchezaji muhimu zaidi kwa Arsenal Msimu uliopita. Picha IB Times.

Kiungo mkabaji pia anahitajika ili kuziba pengo la Mohamed Elneny atakapojiungoa na Misri kwa michuano ya ubingwa kwa mataifa ya bara Afrika mnamo Januari. Pia kuna mwanya mkubwa ambao umeachwa wazi na kuondoka kwa wachezaji wa muda mrefu wa klabu hiyo  Mikel Arteta, Mathieu Flamini na Tomas Rosicky. Mlinzi katika safu ya nyuma atakuwa msaada mkubwa kwa akina Calum Chambers na Per Mertesacker ambao wanaonekana kutatizika mara kwa mara.

Kuna uvumi jijini London kuwa Wenger amekabidhiwa kitia cha pauni milioni 200 ili kukinoa kikosi chake tayari kwa msimu kesho, pesa hizi zikichangiwa na mapato ya kandarasi ya matangazo ya runinga ya msimu ujao. 

Granit Xhaka atakuwa sajili wa kwanza akiwasili kutoka  Borussia Monchengladbach kwa dhamani inayokadiriwa kuwa Euro milioni 43 akisajiliwa kwa mshahara wa pauni elfu 80 kwa wiki kwa kandarasi a miaka mine. Xhaka ataziba mwanya ambao umekuwa chanzo cha klabu hiyo kukosa kustahimili mashambulizi ya kujibiza. Msimu uliopita kiungo mfaransa Francis Coquelin alisaidia kwa kiasi fulani lakini punde tu alipokumbwa na jeraha wakati wa pambano dhidi ya West Brom, wanabunduki tena walizama katika lindi la kuumizwa na wapinzani wenye kasi kama Swanzea na Cryatal Palace.  

Sanchez ndiye mchezaji wa hivi karibuni kusaini mkataba mpya huku pia Ozil akitarajiwa kufuata mkondo baada ya michuano ya ubingwa wa mataifa ya bara Ulaya. Baada ya kutia kapuni windo la Xhaka, straika wa Juventus Alvaro Morata ambaye kwa muda mrefu amefuatiliwa sana na Arsene Wenger anasemekana kuwa shabaha itakayofuata kwa mfaransa huyo. Anakadiriwa kugharimu takriban pauni milon 38 ikiwa klabu yake ya Real Madrid itaamua kumrudisha mchezaji huyo uwanjani Santiago Bernabeu msimu ujao.
Watu wengi wamemsuta kwa idadi ndogo ya mabao aliyoyafunga msimuu uliopita katika ligi kuu Italia lakini ni muhimu kuzingatia kuwa alianza katika mechi  22 tu huku akiingia uwanjani kama nguvu mpya katika michuano 20 na kucheka na nyavu mara tisa na kuchangia mengine tisa.
Vincent Janssen ni baadhi ya washambulizi wanaowindwa na Arsenal. Picha The Telegraph
Inasemekana kuwa Wenger ametuma maskauti kumtazama straika wa klabu ya ligi kuu Uholanzi AZ Alkmaar Vincent Janssen ambaye alitumbukiza mpira langoni mara has 27 katika mechi 34 tangu aisakatie klabu hiyo mechi yake ya kwanza mnamo mwaka 2015. Labda huenda huyu akawa chagua bora kwa bei nafuu. Kaimu meneja wa arsenal Steve Bould pia anapendelea klabu hiyo imsajili mlinzi wa Bolton Wanderers Rob Holding ambaye wachanganuzi wa soka wanamfananisha na mlinzi wa Chelsea Gary Cahill aliyeanzia taaluma yake na klabu hiyo. Chanzo cha hofu kwa usajili huo ni uwezekano wa Chelsea pia kupeleka ofa yao pia wakipania kuwapiku Arsenal vile walivyofanya kwa Cahill.

 Rob Holding ambaye anafananishwa na Gary Cahill huenda akajiunga na Arsenal. Picha www.express.co.uk
Nukuu ya kipa Wojciech Szczesny kuwa alijifunza mengi zaidi akiwa Roma kuliko aliyojifunza akiwa Arsenal ni dhihirisho tosha kuwa yuko radhi kusaini mkataba wa kudumu na miamba hao wa ligi kuu Italia Serie A. Szczesny anakabiliwa na changamoto moja ya kukatwa mshahara ikiwa anataka kufanya mkataba wake kuhamia Roma huwe wa kudumu.  Kama hatakuwa radhi basi itambidi arudi mjini London kumkabili  Petr Cech kuwania nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza.

Wenger pia anataka Theo Walcott asalie na klabu hiyo licha ya kukashifiwa na mashabiki wa klabu hiyo. Mwingereza mwingine Jack Wilshere yuko radhi kutia saini mkataba mpya.
Arsenal ikifanikisha haya yote hawatakuwa mbali na ubingwa.
Share on Google Plus

Kuhusu Unknown

Michezo Kenya Tunapenda Spoti

0 comments:

Post a Comment