Mbona Walcott Alitemwa na Hodgson?



Walcott hatowakilisha Uingereza katika dimba la taifa bingwa barani Ulaya.

 Na Dan Ogega

   Memeja wa timu ya soka ya Uingereza Roy Hodgson ametaja kikosi kitakachowakilisha taifa hilo katika michuano ya taifa bingwa barani Ulaya baadaye mwaka huu. Mwenye amekumbwa na mshangao ni winga wa Arsenal Theo Walcott, ambaye ameachwa nje ya kikosi hicho baada ya msururu wa matokeo duni msimu uliopita.

Sasa Walcott anasema kuwa ameghadhabishwa na hatua hiyo huku akitumia nafasi hiyo kutakia kikosi hicho kila heri katika dimba hilo.

Walcott amechemsha sana msimu uliopita.

"Ni ukweli nimeudhika kwa kutojumushwa kikosini, lakini nimezunguzma na Roy na ninaheshimu uamuzi wake.''

"Nawatakiwa heri njema kule Ufaransa.’’

Pia anaema kuwa anaheshimu uamuzi wa Hodgson akisema kuwa hiyo ni changamoto kwake kuimarisha mchezo wake.

Hatua ya bwana Hodgson inaeleweka kwa sababu Walcott amekuwa miongoni mwa vyanzo vya matokeo mabaya kwa klabu yake ya Arsenal ambayo ilimaliza msimu katika nafasi ya pili, licha ya wao kupewa nafasi kubwa kutwaa ubingwa wa msimu huu. Mashabiki wa klabu hiyo walighadhabishwa na kudorora kwa mchezo wake huku wengi wakimkemea baada ya kuchemsha dhidi ya Crystal Palace. 

Kinda wa Manchester United Marcus Rashford na winga wa Newcastle United  Andros Townsend ni miongoni mwa chipukizi watakaofurahia kuwakilisha Uingereza nchini Ufaransa mbele ya Walcott katika kikosi cha wachezaji 23.
Mwanabunduki mwenzake Jack Wilshere ni mwingi wa furaha baada ya kuitwa na meneja wa timu hiyo licha ya kuwa mkekani kwa muda mrefu msimu uliopita.

 Kikosi kamili

Walindalango: Joe Hart, Fraser Forster, Tom Heaton
Walinzi: Nathaniel Clyne, Kyle Walker, John Stones, Chris Smalling, Gary Cahill, Danny Rose, Ryan Bertrand 

Kipa wa Manchester City Joe Hart ataongoza walinda lango wenzake kikosini

Viungo: Dele Alli, Ross Barkley, Fabian Delph, Eric Dier, Danny Drinkwater, Adam Lallana, Jordan Henderson, James Milner, Raheem Sterling, Andros Townsend, Jack Wilshere 
 
 Jack Wilshere
 
Washambuliaji: Wayne Rooney, Jamie Vardy, Daniel Sturridge, Harry Kane, Marcus Rashford.
Wayne Rooney
 Baada ya msimu wa kufana Rashford amepewa mualiko kikosini
 
 Marcus Rashford

Share on Google Plus

Kuhusu Unknown

Michezo Kenya Tunapenda Spoti

0 comments:

Post a Comment