Na Dan Ogega
Mchezaji wa
klabu ya Chelsea anayechezea klabu ya ligi kuu Ujerumani Bundesliga Werder ameisaidia klabu hiyo
kuhepa shoka la kushuswa daraja baada ya kuwafungia bao la ushindi katika
mchuano wao wa mwisho msimu huu.
Licha ya
bao hilo la dakika ya 88 kushukiwa kuwa lilifungwa wakati mchezji huyo akiwa
ameotea, liliisaidia klabu hiyo kusalia katika ligi ya dara la kwanza huku
wenzao Eintracht Frankfurt wakishushwa daraja.
Ushindi
huo uliiwezesha Weder kuchupa hadi nafasi ya 13 huku Frankfurt wakilazimika
kucheza mchujo wa mikumbo miwili dhidi ya Nurnberg ili kung’amua ikiwa
watacheza Bundesliga msimu ujao.
Wakati
huo huo mabingwa wa ligi kuu Ujerumani mwaka 2007 VFB Stuttgart walishuka daraja moja kwa
moja na wakijiunga na Hannover 96 ambao watacheza ligi ya Bumdesliga 2 msimu
kesho.
Djilobodji
alikuwa sajili wa mwisho wa Jose Mourinho kabla ya kupigwa kalamu mnamo mwezi
Disemba licha ya mreno huyo kusema kuwa hakuwa na habari kuhusu dili hiyo.
Djilobodji baada ya kutia saini kandarasi Chelsea
Aitha alicheza
mara moja akiwa ndani ya jezi ya Chelsea kabla ya kuhamia Bremen kwa mkopo
mnamo Januari.
Werder
Bremen walikuwa katika nafasi ya 16 wakat wa mjo wake ikiwa ni nafasi mbili na
alama mbili nyuma ya Frankfurt when Djilobodji.


0 comments:
Post a Comment