Na Dan Ogega
Katika msimu wa joto wa mwaka 2014 klabu moja ya ligi kuu Uingereza ilikuwa inamhitaji kiungo matata ambaye ana uwezo wa kusababisha mabao na kutia safu za ulinzi za timu pinzani hofu kila mara. Kupitia upekuzi wa kina maajenti wa klabu hiyo wakiorodhesha wachezaji 10 ambao walikuwa na uwezo wa kujaza nafasi hiyo.
Mmoja katika orodha hiyo ni kiungo ambaye
walikuwa wanemuuza katika mwaka uliotangulia na mwingine ambaye hakuwa amecheza
hata mechi moja katika ligi kuu premia. Alikuwa emecheza mechi nane tu katika
ligi ya daraja la pili na kufunga mabao matatu. Na si mwingine bali ni Riad
Mahrez.
Bao lake la ushindi katika mechi
dhidi ya Watford usiku wa jumamosi liliisukuma klabu ya Licester City kileleni mwa jedwali la ligi kuu
Uinereza huku wakifungua mwanya wa alama tano mbele wa Spurs wanaoshikilia
nafasi ya pili. Hilo lilikuwa bao lake la 15 ligini msimu huu licha ya kupoteza
penalty mbili. Huenda meneja wa klabu hiyo Claudio Ranieri anashuku uwezo wa
klabu yake kushinda ligi kuu lakini hali ya mchezaji huyu anayeibukia Aljeria
inaweza kuwa kidhibitisho tosha kwa muitaliano kuwa kushinda ligi sio chaguo
tena bali ni jambo la lazima.
Mahrez baada ya kuifungia Leicester mabao matatu.
Mahrez baada ya kuifungia Leicester mabao matatu.
Klabu yake ya zamani ya Quimper
Kerfeunteun FC, inayoshirki ligi ya daraja la saba katika taifa la Ufaransa
huenda ikanufaika na takriban pauni 20, 0000 ikiwa atauzwa kwa kima cha pauni
milioni 40. Hili linatilia mkazo safari ya mchezaji huyu ambaye hadi msimu jana
ni mashabiki wachache sana wangebashiri
kuwa angefikia kiwango hiki cha ufanisi.
“Tumetaniana sana kuhusu hilo hapa.
Lakini iwapo litatendeka basi litakuwa jambo la maana sana kwetu.’’ Alisema mkurugenzi
wa kitengo cha watoto cha klabu hiyo.
Riad akicheza kule Ufaransa
Riad akicheza kule Ufaransa
Kinyume na hali ya kinda Ousmane
Dembélé, ambaye ni chipukizi wa hivi punde tu kung’ang’aniwa na vilabu vingi
barani ulaya, Mahrez hakujifunza soka katika akademia yoyote jambo ambalo
linaleta hali ya kutotabirika ya mchezo wake.
“Sisi hatujaratibiwa.ukiwa, katika kiwango cha
akademia inabidi uingie mazoezini kila
siku saa tatu asubuhi. Fanya hili fanya lile. Lakini kwangu naamini kuwa soka
ya mitaani huleta nyenzo fulani katika timu.’’
Huenda sogora huyu hangejulikana
kama si simu ya meneja Nzete Ate na pia mkuu wa kitengo cha kugundua talanta
katika klabu ya FC Nantes Mathieu Bideau. Ate alikuwa amemshuhudia Mahrez akiimarika
tangu akiwa mdogo huku jambo lililomvutia kwake ni bidii na uchu wa kuimarika
kila uchao. Wale wanaomkumbuka akiwa mitaani Sarcelles wanasema kuwa alikuwa
akifanya mazoezi hadi majira ya saa nne usiku na kurauka tena saa kumi
alfajiri.
Bideau alimwarifu Mickaël Pellen,
ambaye ni kaimu mkufunzi katika klabu ya Quimper ambaye alimwalika katika zoezi
la majaribio lililohusisha wachezaji 25.
“Ni mimi pekee niliyesalia baada ya
majaribio hayo. Mahrez aliliambia jarida la Cote Quimper mnamo mwaka 2012.
“Meneja Ronan Salaun aliniamini licha ya kuwa
sikujumuishwa katika kikosi cha kwanza katika kipindi cha miEzi sita ya kwanza.
Lakini ilikuwa klabu nzuri ambayo ilikuwa inazingatia maadili ya kifamilia na
nina kumbukumbu nzuri kwa wakati wangu huko.
Pia ilinisaidia kukua kimawazo kwani ndio ulikuwa wakati wangu wa kwanza
kukaa mbali na familia yangu.''
Safari yake katika soka ilikubwa na changamoto
kibao kwani kutokana na tambo lake dogo hakuna meneja aliyekua na nia ya
kusajili.
Wakufunzi wake wote wanamzungumzia
kama mchezaji aliyekuwa na kiu ya kujifunza na kujua mengi kuhusu uchezaji wa
soka bila kukorofishana na yeyote yule.
“Alikuwa na uhakika angekuwa profeshenali
wakati mmoja licha ya ukweli kuwa wengi walimpuuza. Kwa upande wake hakujishuku
hata kidogo.’’ Mohamed Coulibaly alinukuliwa akimuongelea Riad.
Mwisho wa msimu wa mwaka 2009 Mahrez
aliondoka Sarcelles huku akimwahidi Coulibaly kuwa alidhamiria kucheza katika
dimba la kombe la dunia la mwaka 2014 nchini Brazil.
Mnamo Mei 2014 mwezi mmoja kabla ya
dimba hilo kungoa nanga aliitwa kwa mara ya kwanza kuchezea mbweha wa jangwani
huku akiorodheshwa miongoni mwa wachezaji 23 walioikalifisha Ubelgij mabao 2-1.
Mahrez alijifunza kuzoea kwa haraka mazingira mageni kule Quimper alipokuwa akiishi chumba kimoja na kakake Pul Pogba Mathias. Wote walikuwa walikuwa wakilipwa pauni 750 kwa mwezi. Mwaka mmoja baadaye alihamia Le Havre pahali ambapo alikumbana na uhalisia kuwa akademia ya klabu hiyo ilikuwa ikiwachomoa chipukizi walio na talanta za hali ya juu. Huko pia ilimchukua msimu mmoja kuingia katika kikosi cha kwanza.
Mchuano muhimu kabisa katika taaluma
yake ulifanyika mnamo tarehe 14 mwezi Septemba mwaka 2013 ambapo alifunga bao
moja na kuchangia mengine matatu katika
ushindi wa 6-2 dhidi ya Le Havre. Katika
kipindi cha miezi sita klabu yake
haikuwa imesajili ushindi hata mmoja.
Hadi sasa yeye hushikilia msimamo
mmoja.
“ Fikira zangu kijumla kuhusu soka
ni kuwa ni nafasi ya kujiburudisha. Hadi sasa mimi hufuata fikira hizi za
kutojali.’’ Alinukuliwa na jarida NewsOuest.
Maisha yake yanazingirwa na
kujiamini, kutokufa moyo, kufuata masharti na pia kuwa na hari na uchu wa
kujifunza. Taji la mchezaji bora aliloshinda msimu huu ni matunda ya haya yote.

0 comments:
Post a Comment