N'Golo Kante akiwajibikia Leicester City
Na Dan Ogega
Huenda klabu ya Arsenal imeamua kutowazingua
tena wafuasi wake msimu ujao baada ya kuafikia makubaliano ya kumsajili kiungo
mkabaji wa Leicester City mfaransa N’Golo Kante. Habari ambazo zimezagaa katika
majarida ya Ufaransa ni kuwa Kante ameridhia kuhamia London msimu ujao.
Kante
ambaye alijumuishwa katika kikosi cha msimu uliopita katika ligi kuu Uingereza baada ya kuisaidia Leicester kushinda taji la Uingereza, anakadiriwa
kugharimu Arsenal kitita cha pauni milioni 20. Aitha anasemekana kuvutiwa na
mfumo wa meneja Arsene Wenger na pia uhusiano wake mzuri na wacheaji chipukizi.
Mchezaji huyo
amekuwa akihusishwa pakubwa na kuhamia London huku kituo cha televisheni cha French TV kupitia kipindi chaTelefoot kikifichua
kuwa uvumi huo huenda ukawa ukweli katika siku za usoni.
Vyanzo vingine
vinasema kuwa wakala wa Kante amekutana na wawakilishi wa wanabunduki hao ili
kufuma dili hiyo kikamilifu.
N'Golo
Kante pia amehusishwa na vilabu kadhaa vikiwemo Manchester United na Manchester
City lakini meneja mpya wa City Pep Guardiola anasemekana kutopendezwa na
uchezaji wa mfaransa huyo.
Kante
atashiriki michuano ya taifa bingwa bara ulaya na timu ya Ufaransa.

0 comments:
Post a Comment