Onyo la Tusker kwa Gor




  Mabingwa ligi kuu ya Kenya Gor Mahia wameonywa dhidi ya kuwanyemelea wachezaji wa Tusker Eugene Asike na Humphrey Mieno, kwani wako na mikataba na klabu hiyo kwa sasa.
Haya ni kulingana na mkurugenzi mkuu wa wanamvinyo Tusker Charles Obiny ambaye anasisistiza kuwa lazima K’Ogallo ifuate taratibu husika ikiwa inataka kuwasajili wawili hao.
 “Hadis sasa hatujazungumza na wakala au mwakilishi yeyote wa klabu kuhusu uhamisho wa wachezaji hao. Ikiwa wanahitaji huduma zao lazima wazingatie sheria na taratibu husika. Kwa sasa hatuko tayari kumpoteza mchezaji wowote katika kipindi hiki cha uhamisho kwa sababu tuna nia ya kuwinda taji la ligi kuu msimu huu.’’ Mkurugenzi huyo alinukuliwa na vyombo vya habari.
Mwenyekiti wa Tusker James Musyoki pia amekariri kauli hiyo huku akisema kuwa hawana nia yoyote ya kuachilia mchezaji hata mmoja.
 “Nina habari kuwa kuna vilabu vinataka kunyakuwa wachezaji wetu lakini sitaki kumwachilia mchezaji yeyote kwa sasa. Kwa sasa tuna lengo la kunyakua taji la ligi kuu msimu huu kwa sababu tumetathmini na kung’amua kuwa hakuna mpinzani yeyote aliye na ubora kama wetu msimu huu.” Alisema Musyoki.
Asike amekuwa tegemo kwa wanamvinyo hao msimu huu bada ya kujiunga nao mezi Juni mwaka jana akitokea Sofapaka huku mchezo wake wa kumakinika ukimsaidia kutajwa tena katika kikosi cha timu ya taifa Harambee Stars.
Kwa upande Mieno amekuwa kiungo muhimu kwa Tusker msimu huu huku ushirikiano wa hao wawili hao ukiipaisha klabu hiyo hadi kileleni mwa ligi kuu.
Nahodha wa Tusker James Situma ameutaka usimamizi wa klabu hiyo kutoridhia uhamisho wowote kwani hatua hiyo huenda ikawabomoa.
 ‘Nimezungumza na mamlaka na kuwajuza umuhimu wa kuwasaza wachezaji muhimu klabuni. Halitakuwa jambo la busara kuwaachila wachezaji katika hatua hii kwani huenda timu ikalegea.
Wakati huo huo ni kuwa Tusker itahamia uwanja wake wa nyumbani wa zamani Kinoru kwanzia mechi ya kwanza ya awamu ya pili msimu huu ambapo watapambana na Rangers.

Share on Google Plus

Kuhusu Unknown

Michezo Kenya Tunapenda Spoti

0 comments:

Post a Comment