'Celebrities' 10 Watakaosimama na Real Madrid Katika Fainali

Huenda klabu ya Real Madrid ikafungua ukurasa mpya katika historia ya klabu bingwa barani ulaya ikiwa watawafunika au kuwapokeza vigongo wadogo zao na wapinzani wa jadi kutoka jiji la Madrid Atletico,  kwani litakuwa taji la 11 kwa klabu hiyo, idadi ambayo ni kubwa zaidi kwa klabu yoyote. Mchuano huu utawautanisha wapinzani ambao wana utani na ubishi mkubwa zaidi katika derby zote nchini Uhispania ambao walipatana tena katika fainali ya msimu wa 2013/14, huku Los Blancos wakiwafumua Rojiblancos goli 3-1.

Mchuano huu pia umezua ubishi miongoni mwa watu tajika ulimwenguni almaaruf celebrities ambao bila shaka watavalia jezi maarufu za klabu zao ili kuwapa motisha.

Mwigizaji maarufu wa filamu Jennifer Lopez amezuru uwanja wa Santiago Bernabeau mara kadhaa kitika siku za nyuma na hakuna shaka kwamba kesho atajumuika na wafuasi wenzake wanaojitambua kama Madridistas ili kuwapiga jeki Real Madrid. 

Actor tajika wa Hollywood Slyvester Stallone A.K.A Rambo anatambulika kwa mapenzi yake kwa Los Galacticos baada ya kununua jezi ya klabu hiyo iliyobandikwa jina 'Stallone' kwenye mgongo.

Mcheza tenisi Martina Hingis ni maarufu miongoni mwa wapenzi wa Real baada ya kuhudhuria mchuano wa mkumbo wa pili katika ya klabu hiyo na Manchester City katika unwanja wa Bernabeau katika awamu ya nusu fainali msimu huu.

Julio Jose Iglesias de la Cueva ambaye ni mwimbaji nchini uhispania alikuwa mlinda lango wa Real Madrid kabla ya kutundika daluga zake. Anajulikana sana kwa kupendelea jezi nambari 12 ya klabu hiyo ambayo inavaliwa na Marcelo Santos Jr kwa sasa.

Nguli wa mchezo wa tenisi nambari moja duniani Mhispania Rafael Nadal kamwe hajawahi kudhibiti hisia zake kuhusu Real Madrid. Kwa mara zaidi ya moja ameonekana akiwa ndani ya pamba nyeupe ya Los Galacticos.

Mwimbaji mwingine mwenye damu ya kimadridista ni Malu ambaye atakuwa akishabikia Madri katika fainali ya mwaka huu mjini Milan Italia.

Kama ushawahi kutazama filamu kwa jina Night at the Museum basi unamfahamu mwuguzaji mkuu Ben Stiller. Huyu bingwa ni mpenzi wa dhati wa Real Madrid.

Mwimbaji wa muziki aina ya Pop ambaye pia ni mchumba wa kipa wa Manchester United
Edurne Garcia, amekuwa akimrai kila uchao kipa huyo kuamia Madrid bila mafanikio. Wakati mmoja alijipata pabaya baada ya kuweka bayana chuki zake kwa klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu Uingereza.

Rais wa Uhispania Marian Rajoy ni miongoni mwa watu tajika ambao wanajulika na kwa kuenzi  klabu ya Real Madrid. 

Share on Google Plus

Kuhusu Unknown

Michezo Kenya Tunapenda Spoti

0 comments:

Post a Comment