Mchezaji bora zaidi katika kikosi cha Arsenal Mesut Ozil huenda akahama klabu hiyo msimu ujao ikiwa the gunners hawatashinda taji lolote. Hii ni baada yake kukataa kutia saini kandarasi mpya na klabu hiyo huku akisema kuwa hataki kujibana na klabu hiyo ikiwa matokeo yake hayataimarika msimu ujao. Arsenal ilikuwa tayari kumpa mkataba wa pauni elfu 200 kwa wiki ili aongeze muda katika kandarasi yake ya sasa lakini mjerumani huyo anadai kuwa pesa sio tatizo kwake bali ushindi wa mataji.Kwa sasa majarida kadhaa ya kule Uingereza yanadai kuwa mchezaji huyo amevutiwa na klabu nyingi kubwa ambazo zimedhihirisha nia ya kutaka huduma zake.
Wakati huo huo mabingwa wa ligi kuu Italia Serie A Juventus wanajiandaa kuachana na mshambulizi wake Mhispania Alvaro Morata huku meneja wa klabu hiyo Maximiliano Allegri akisema kuwa wanajianda kwa maisha bila straika huyo. Arsenal inajiandaa kupelEka ofa ya kima cha pauni milioni 24 ili kumnyakua mchezaji huyo ambaye ni zao la aakademia ya klabu ya Real Madrid.
“Klabu inaendelea kutafuta wachezaji mbadala katika soko lakini sio rahisi kupata wachezaji wa kiwango cha juu kwa sasa,” Allegri aliiambia runinga ya Sky Italia.
“Kwa sasa tuna washambulizi wengi wachanga ambao idadi kubwa inachezea vikosi vya mataifa yao.”
“Nishazungumza na Morata na nikamuelezea kuhusu umuhimu wak kusalia nasi. Na nina imani ananielewa .”

Beki wa klabu hiyo Hector BellerĂn anafuatiliwa kwa karibu na klabu yake ya zamani ya FC Barcelona ambayo inatafuta atakayeziba pengo la Dani Alves ambaye anatarajiwa kujiunga na miamba wa Italia Juventus.
Barca iliibukia habari za kutamausha mnamo Jumatano kuwa wachezaji wao muhimu Javier Mascherano na Alves walikuwa washakubaliana na Juventus kuhusU uhamisho lakini muajentina huyo amekana madai hayo.

Kwa sasa the catalans hawana wasi wasi kuhusu Mascherano kwa sababu mkataba wake unatamatika mwaka 2017 lakini kuna uwezekano mkubwa Alves akondoka Nou Camp kwa sababu kuna kipengele katika mkataba wake kinachomrhusu kuhama msimu ujao.
0 comments:
Post a Comment