'Celebrities' 10 Watakaosimama na Atletico Madrid Katika Fainali ya UCL

Atlectico Madrid wamekuwa mwiba kwa klabu kubwa msimu huu katika michuano ya ubingwa wa klabu barani Ulaya baada ya kuwapinga nje ya ubingwa huo mabingwa watetezi FC Barcelona na FC Bayern Munich katika awamu ya robo fainali na nusu fainali mtawalia. Hivyo basi sio muujiza kuwa Rojiblancos wanashiriki fainali kwa mara ya pili katika muda wa miaka mitatu wakiongozwa na muajentina Diego Simeoni. Hawa ndio watu maarufu duniani ambao watakuwa ndani ya jezi ya michirizi ya rangi nyekundu na nyeupe kwenye jukwaa la mashabiki kule San Sir, Milan Italia.

 David Munoz ni mpishi hodari mjini Madrid lakini kamwe hajawahi kuvutiwa na Real Madrid na badala yake anaipendelea sana Atletico.

Pedro Sánchez Pérez-Castejón  ni mwanasiasa na katibu mkuu wa chama cha Spanish Socialist Workers' Party tangu mwaka 2014. Kando na masuala ya siasa yeye ni mpenzi wa dhati wa Atletico. 

Cayetano Luis Martínez de Irujo ni mkimbiza farasi tajika nchini Uhispania ambaye kwa siku za nyuma ameonekana katika uwanja wa nyumbani wa Atletico Vicente Calderon akifuatilia matokeo ya klabu yake. 

Jose Tomas ni mchezaji wa zamani wa klabu ya Atletico ambaye mapenzi yake hayakuisha baada ya kutundika daluga zake. Hadi leo anazidi kufuatilia klabu yake kwa karibu sana. 

Rosendo Hernández González ni sampuli ya Diblo Dibala wa kule Uhispania mbaye penzi lake katika kupiga gitaa pia limepenya mipaka hadi kwa soka. Kwa wakati mwingi yeye hutumbuiza washikaji akiwa na jezi ya Rojiblancos. 

Ana Rosa Quintana ni matngazaji maarufu kule Uhispania ambaye ni nadra kuonekana mitaani akiwa ndani ya rangi tofauti na ile ya jezi ya Atletico Madrid. 

Luis de Guindos ni waziri wa biashara nchini Uhispania na bila shaka alisumbuliwa sana masaibu ya kifedha ya klabu ya Atletico Madrid katika siku za nyuma. Pia aliwakilisha taifa la Uhispania katika mazungumzo ya kunusuru uchumu wa taifa la Ugiriki mwaka jana. 

Álvaro Bautista Arce ni mwendesha piki piki maarufu duniani na yeye amebandika rangi za Atletico katika mtambo wake wa mashindano pia pamba zake.

Mwimbaji Dani Martin ni miongoni mwa wanamuziki lukuki wanaoshabikia Atletico Club de Madrid.


Joaquín Sabina ni mwandishi mwenye cheo cha juu nchini uhispania lakini fikra kuhusu klabu ya Atletico huwa naye wakati wowote.
Share on Google Plus

Kuhusu Unknown

Michezo Kenya Tunapenda Spoti

0 comments:

Post a Comment