Ni Nani Atashiriki Champions League?

City, Liverpool na Arsenal wanang'ang'ania nafasi tatu zenye uhakika wa kucheza Ulaya msimu ujao
    

Arsenal wakiingizwa kwenye droo mwaka jana.
  
Na Dan Ogega
   Ni bayana kuwa sasa ubishi kuhusu mshindi wa taji la ligi kuu premia Uingerera ushazikwa katika kaburi la sahau baada ya Chelsea kutoshana nguvu na Spurs mapema juma hili, jambo lililopelekea Leicester kutawazwa mabingwa wa msimu huu. Pia ni vigumu kuamini kuwa bingwa mtetezi Chelsea hayupo miongoni mwa timu zitakazowakilisha Uingereza katika kipute cha ubingwa wa vilabu barani Ulaya msimu ujao. Lakini huenda wakafuzu kushiriki ubingwa wa taji la Europa League licha ya kusajili matokeo duni msimu huu.

   Ikiwa watawapiku wapinzani wao katika michuano iliyosalia huenda wakamaliza katika nafasi ya saba hali ambayo itawatuunuku nafasi ya kujifuta machozi kwa kupambana katika ligi la Europa msimu kesho. 



Chelsea huenda wakashiriki Europa msimu kesho

   Kulingana na kanuni za sasa, klabu zinazomaliza ndani ya nne bora zitafuzu moja kwa moja huku timu zitakazomaliza katika nafasi za tano na sita zitashiriki Europa League. Pia huenda washindi wa kombe la Capital One Manchester City wakamaliza katika nafasi ya tano na Manchester United wamalize msimu wakiwa ndani ya sita bora na pia kushinda kombe la FA Cup. Katika mazingira haya basi itabidi timu itakayomaliza katika nafasi ya saba ifuzu kuingia Europa League. Hii ni kwa sababu washindi wa mataji ya nyumbani wanafuzu moja kwa moja kushiriki michuano ya Europa League.


Arsenal wako hatarini kutoshiriki UCL msimu ujao 

   Ikifanyika kuwa miamba wa Liverpool wameutwaa ubingwa wa mwaka huu wa dimba la Europa League, basi Uingereza itawakilishwa na klabu tano katika dimba la UEFA Champions League msimu kesho ikiwajumuisha Liverpool wenyewe.

   Lakini ikiwa the reds watashinda fainali ya mwaka huu na kumaliza katika nafasi za tano sita au saba basi nafasi hiyo haitatunukiwa klabu za Uingereza. Hali hii itapelekea Uingereza kuwakilishwa na klabu tano katika ubingwa wa ulaya na pia timu mbili katika dimba la Europa League.


Ndoto ya Uingereza ilizimwa na Real Madrid

  Ushindi wa Real Madrid dhidi ya Man city ulifuta uwezekano wa timu kumaliza kaika nafasi ya nne na kushiriki Europa League. Pia ingefanyika kuwa City na Liverpool zingeshinda mataji ya Europa League na UEFA Champions League na kumaliza ndani ya nne bora basi zote zingeshiriki Champions League pamoja na wawakilishi wengine watatu watakaomaliza ndani ya tatu bora.

Share on Google Plus

Kuhusu Unknown

Michezo Kenya Tunapenda Spoti

0 comments:

Post a Comment