Nemanja Matic na Jose Mourinho wana uhusiano mwema
Na Dan Ogega
Meneja Mpya mtarajiwa wa Manchester United Jose
Mourinho hatachukua muda mrefu kuimarisha kikosi chake, kwani atavamia kambi ya klabu yake ya zamani Chelsea akizisaka huduma za
kiungo mkabaji mserbia Nemanja Matic katika harakati za kwanza za kutumia mtaji
wa pauni milioni 200 atakazopokezwa na wamiliki wa Manchester United. Mourinho
anapendelea kipaji cha mchezaji huyo ambaye alimrejesha Stamford Bridge kutoka
Benfika kuliko wachezaji waliomo kikosini kama Moruane Fellaini na Michael Carrick,
ambao wameorodheshwa kama vyanzo vya mashetani wekundu kuchemsha katika siku za
nyuma. Inakisiwa kuwa Matic ataigharimu United kitita cha pauni milioni 25.
Pia the
special one kama anavyojitambulisha mreno huyo atapeleka toleo Everton kwa
ajili ya kumnasa mkabaji wao John Stones ambaye anakadiriwa kugharimu kima cha pauni
milioni 45, huku pia mkondo wa pili ukimuelekeza Madrid ambapo takriban pauni
milioni 35 zitakuwa tosha kumtia kapuni mfaransa Raphael Varane.
Wakati huo huo kiungo wa United Mhuspania United Juan Mata ataandaa
mazungumzo na Mourinho ili kumuelezea mreno huyo nia yake ya kusalia Old
Trafford, wakati mhispania mwengine kipa David de Gea akikisiwa kujianda kusepa
kuelekea Real Madrid.
Katika kipindi
chake kama mkufunzi huko Chelsea Mourinho alimponza Mata kabla ya kuamrisha
kuuzwa kwake kwenda Manchester United mnamo Januari mwaka 2014 kwa dhamani ya
pauni milioni. Vyanzo vya habari kutoka Manchester vinasema kuwa Mata yuko
tayari kurudiana na meneja wake wa zamani huku akisistiza kuwa kamwe hajawahi
kukosana na Mourinho.
Hatua ya
kumteua Mourinho kama meneja mpya wa klabu ya Manchester United ni jambo la muda
tu baada ya Mholanzi Luis Van Gaal kupigwa ufagio wa chuma mapema juma hili. Kitendo
hiki kinatarajiwa kuleta mwanzo mpya baada ya uchezaji chwara klabu hiyo imekuwa
ikidhihirisha katika siku za nyuma tangu kuondoka kwa kocha wa zamani wa klabu
hiyo Mskochi Sir Alex Ferguson.

0 comments:
Post a Comment