Chanzo cha Vifo Uwanjani





Hii ni sehemu ya pili ya maelezo kuhusu tatizo la mshtuko wa moyo inayopania kufafanua na kuelimisha umma kuhusu zogo hili. 

... ‘‘Kwa nini tunatakiwa kung’amua? Kwanza inasaidia kutofautisha kati ya msukumo wa damu na maradhi ya mshtuko wa moyo. Daktari Larose anaendelea kuelezea.

 “Mshtuko wa moyo hutokana na matatizo ya mishipa,” anaelezea Chris Simpson, ambaye ni tabibu mkuu wa katika hospitali ya chuo kikuu cha Queen nchini Uingereza. 

 
 Mchezaji wa Bolton Wanderers Fbrice Muamba baada ya kuzirai.
 
‘‘Mshipa unaopeleka damu kwa moyo huzibwa kutokana na kujazana kwa mafuta aina ya cholesterol, hali inayosababisha sehemu ya moyo inayohudumiwa na mshipa huo kuharibika.’’

 “Mshtuko wa moyo ni tatizo linaloweza kufananishwa na umeme,” anazidi kufafanua daktari Simpson. 

“Mapigo ya kawaida ya moyo yanayosababisha  mdundo wa moyo huathirika na kupelekea moyo kusimama na kutulia. Wakati mwingine mapigo haya huweza kuwa ya haraka au pole pole zaidi ya idadi ya kawaida. Hali hii inaweza kusababisha moyo kuzima ghafla.

 
 Mshtuko wa moyo unaweza kufananishwa na mawimbi ya umeme

Baadhi ya visa vingi vya mshtuko wa moyo huletwa na matatizo ya kiafya ambayo hurudhiwa kutoka kwa wazazi kama Long QT Syndrome, Brugada Syndrome, Catecholaminergic Polymorphic Ventricular Tachycardia, Arrhythmogenic Right Ventricular Cardiomyopathy na hypertrophic cardiomyopathy.

Matatizo haya yanaweza kuwa magumu kugundua lakini ukichunguza idadi kamili ya watu waliofariki baada ya kudondoka ghafla, zaidi ya nusu hudhihirisha ishara za maradhi sampuli hii.

Baadhi ya ishara hizi ni pamoja na kusinzia au kuzimia wakati wa vipindi vya mazoezi. Hii inaweza kuashiria kuwa moyo wa muathiriwa umenza kudunda Zaidi ya kiwango kabla ya kurejelea hali ya kawaida upesi.

Kuzirai kutokana na sauti kubwa  au hofu hali ambayo inaweza kuhusishwa na maradhi ya Long QT Syndrome.

Fabrice Muamba akisaidiwa na wenzake baada ya kuzimia ghafla katika pambano dhidi ya Tottenham kwenye awamu ya tatu ya kombe la FA.

Kama familia ya mwathirika ina historia ya kusimia ghafla katika umri mdogo.
Haya yote yanaweza kuzuiliwa ikiwa vipimo vya kutosha vitachukuliwa na pia hatua mwafaka kuzingatiwa.
Share on Google Plus

Kuhusu Unknown

Michezo Kenya Tunapenda Spoti

0 comments:

Post a Comment