Nitashabikia Arsenal




   Na Dan Ogega

   Mkufunzi  wa Manchester United Luis van Gaal anaamini kuwa klabu yake iko imara katika harakati za kutafuta nafasi ya kucheza michuano ya ubingwa barani ulaya msimu ujao. Ameyasema hayo baada ya United kuilaza Norwich City 1-0.

Ushindi huo umewawezesha kukata uongozi wa Arsenal hadi alama moja. 

Katika kauli ya kushangaza LVG kama anavyojulikana miongoni mwa wafuasi wa klabu hiyo amesema kuwa ataishabikia Arsenal katika pambano la kesho. 

 "Mimi ni shabiki sugu wa Arsenal kwa mchuano wa kesho''

"Lakini nabashiri kuwa utakuwa mgumu hasa ikizingatiwa kuwa City walipoteza dhid ya Madrid.''

"Ni lazima tuzidishe shinikisha kwa wapinzani wetu na tuna uhakika kuwa tutamaliza ndani ya nne bora ili tucheze UEFA msimu kesho.''

United watamenyana na Westham katika pambano lao la mwisho msimu huu na LVG anajua kuwa nchuano huo utakuwa wa kukata na shoka.

" Kwa ukweli ni wagumu hasa ikizingatiwa kuwa kushamenyana nao katika kipute cha FA.'' 

Huenda United wakashiriki Europa League ikiwa watashindwa kumaliza ndani ya nne bora.
Share on Google Plus

Kuhusu Unknown

Michezo Kenya Tunapenda Spoti

0 comments:

Post a Comment