Alexis Sanchez yuko mbioni kuhama Arsenal baada ya kuchoka na maisha katika klabu hiyo. Aitha anaripotiwa kukimbia nje ya uwanja punde tu baada ya kupumzishwa dhidi ya Crystal Palace.
Arsenal wanamyemelea straika wa klabu ya AZ Alkmaar Vincent Janssen aliye na umri wa miaka 21 ambaye alifunga bao la ushindi dhidi ya Aingereza mnamo mwezi Machi.Wakati huo huo Mikel Arteta atajiunga na benchi la kiufindi la klabu ya Manchester City punde tu Pep Guardiola atakapowasili Etihad.
Wakala wa kiungo wa Juventus Paul Pogba amekana uvumi kuwa huenda mfaransa huyo akamfuata Antonio Conte kwa kujiunga na Chelsea.
Barcelona na Chelsea wanammezea mate mchezaji wa zamani wa klabu ya Newcastle Hatem Ben Arfa ambaye anapania kuibua taaluma yake upya.
Mkufunzi wa zamani wa klabu ya Liverpool Brendan Rodgers atarejea Swansea klabu aliyoiongoza kati ya mwaka 2010 na 2012 huku akitarajiwa kupokea mshahara wa pauni elfu 90 kwa wiki.
Liverpool watamwachilia kinda wao Jordan Rossiter aliye na umri wa miaka 19 kujiunga na Rangers wakati mkataba wake utakapokamilika
Watford watamnunua straika wa West Brom Saido Berahino, ili kuziba pengo la Odion Ighalo ambaye anatarajiwa kugura klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Huenda michuano ya UEFA Champions League ikasakatwa wikendi ikiwa chama hicho kitakubali mapendekeza ya kubadilisha ratiba ya michuano hiyo.
0 comments:
Post a Comment