City Hawana ''Company!''



Je City watawahi Madrib Bila Kompany

Na Edwin Mwangi

Nahodha wa Man City amewarai wachezaji pamoja na mashabiki kuwa pamoja watakapo wakabiri Madrid ugani Etihad.
City wanawaribisha mazimwi hao wa Liga kwa mechi ya ufunguzi wa mkondo wa nusu fainali yao ya kwanza katika dimba la Champions League leo Jumanne  baaa ya kuwaangusha Paris Saint-Germain kwenye kikosi cha nane bora

Kevin De Bruyne alikuwa mshindi wa City baada ya kufunga bao la uamuzi la 1-0 dhidi PSG mapema mwezi huu. Kompany amesema kuwa kabla ya mechi kuanza kwamba  niwakati mwafaka wa kikosi cha Pellegrini kupata upato na upeo wa juu.

"Natamani kucheza mchezo bora kesho lakini tunatarajia makubwa kutoka kwa wachezaji wenzetu," alisema beki huyo wa kati.
"Nafikiri tuna msukumo moja . Hatuwezi shindwa kufikia kiwango chetu bora.

" Kucheza dhidi ya wachezaji hao wa hadhi, hilo ndilo tunalolitaka. Na hakuna siku  hata moja kwa maisha yangu nimewahi kufikiria kuwa haya yanaweza nitia wasi wasi au kuwa ngumu. Nataka hili mimi mwenyewe na wachezaji wote wanataka hili. 

Mabingwa hao wa ligi kuu watapata motisha kutoka kwa mashabiki wa nyumbani Manchester na Kompany anaamini kwamba kuwa mashabiki watakuwa na jukumu kubwa sana kwa kuwatia joto.
Hata hivyo kuna tashwishi kwamba Kompany atakuwa kikosinibaada ya kuuguza jeraha la misuri ya mguu lakini hilo halimbabaishi kamwe.
Share on Google Plus

Kuhusu Unknown

Michezo Kenya Tunapenda Spoti

0 comments:

Post a Comment