
Chipukizi wa AFC Leopards wkisherekea bao dhidi ya Gor Mahia. Waliilaza Gor Mahia mabao 2-0
AFC Leopards waliicharaza Gor Mahia mabao 2-0 katika dimba la wachezaji wasiozidi umri wa miaka 20 katika uwanja wa kimataifa wa Nyayo jijini Nairobi.
Mchuano huo ulingoa nanga wa vishindo na makeke ya aina yake huku pande zote mbili zikikosa nafasi za wazi chungu nzima. Waliokosa nafasi ni pamoja na Jack Bruno AFC Leopards kunako dakika ya pili huku dakika tatu baadaye mchezaji mahiri wa K'Ogallo Wilson Mwendwa akikosa lango kwa kichwa.
Mathen Kono akiwapatia kiamsha kinywa kinda wa Ingwe baada ya kumalizia jitihada za klabu hiyo kwa njia maridadi
Shinikizo kutoka Gor kulimpeleka Daniel Odhiambo kuuelekeza mpira langoni mwake lakini jitihada za walinzi wenzake ziliitoa hatari hiyo. Wimbi la kukosa nafasi za kufunga ziliendelea huku Jack Bruno akikosa nafasi ya kuuzidisha uongozi wa AFC Leopard katika dakika ya 30. Dakika saba baadaye Philip Odhiamboaliwahakikishia ingwe ushindi baada ya kutumbukiza wavuni mpira taratibu.
0 comments:
Post a Comment