Mkufunzi wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger anaamini kuwa kiungo wa kati wa taifa la Uingereza Jack Andrew Wilshire yuko fiti kushiriki michuano ya Euro mwaka huu nchini Ufaransa.
Hadi sasa Wilshire hajashiriki mchuano wowote msimu huu baada ya kukumbwa na jeraha la mguu msimu uliopita. Wenger anaamini kuwa mchezaji wake atakuwa dhabiti kuisaidia Uingereza katika michuano ya ubingwa wa bara ulaya kwa mataifa. Juma lililopita alicheza mchuano wake wa kwana katika pambano la chipukizi wasiozidi umri wa miaka 21.
Hivi majuzi tu alinukuliwa akisema kuwa iwapo meneja wa Uingereza Roy Hougson ataamua kumwita Wilshere hautakuwa mchezo wa bahati nasibu.
'Ndio atakuwa vizuri kushiriki Euro kwa sababu amecheza mara tatu katika mechi za vijana wasiozidi umri wa miaka 21.'
'Michuano ya Euro inang'oa nanga tarehe 10 mwezi wa Juni na hadi hapo ni miezi miwili. Ukiangalia hali yake ya mchezo wakati huu, naaminI kuwa atakuwa tayari kwa uda wa miezi miwili.Kama hakutakuwa na viwaz vyovyote basi atakua imara.' Wenger alinukuliwa na wavuti rasmi wa klabu ya Arsenal
Hodgson anatarajiwa kutaja kikosi cha wachezaji 23cha Uingereza mnamo tarehe 12 mwezi Mei..
0 comments:
Post a Comment