Na Dan Ogega
Mjadala kuhusu nani bora zaidi kati
ya Cristiano Ronaldo na Lionel Messi umetamalaki vyombo vya habari kwa muda
mrefu sasa. Wawili hao wameshinda mataji manane ya mchezaji bora duniani kati
yao katika muongo mmoja uliopita jambo lililowafanya wengi kuamini kuwa hakuna
mchezaji atawahi kuibuka na kuwapiku katika ufanisi huo.
Kando na mjadala huu ambao kamwe
huwezi bainisha mbivu na mbichi ni muhimu kuzingatia kuwa kinda mbrazil Neymar
Santos ana miaka mingi ya kucheza kabumbu na pia ana talanta na uwezo wa
kusawazisha au hata kuwapiku wawili hao.
Akiwa na umri wa miaka 23 Neymar amepachika
mabao 183 akichezea vilabu vya Santos, Barcelona na timu ya taifa ya Brazil,hii
ikiwa ni kadri ya mabao 0.57 kwa kila pambano
Wakiwa katika umri huo huo Messi
alikuwa amecheka na nyavu mara Messi 150 huku Ronaldo akiliona lango mara 118.
Neymar pia yuko mbioni kuvunja
rekodi ya kuwakilisha Brazil mara nyingi na pia kuwa mfungaji bora wa vijana wa
Samba.
Hadi sasa amesalia kuchezea Brazil
mara 76 ndio asawazishe rekodi ya veterani wa taifa hilo Cafu aliyeshuka dimbani
mara 142 akiivaa jezi ya Samba na pia akifanikiwa kufunga mabao 31 zaidi
atakuwa ameichakaza rekodi ya nguli wa soka duniani Edson Arantes do Nascimento
almaarufu Pele katika chati za wafungaji bora Brazil.

0 comments:
Post a Comment