Neymar Kuhama Barcelona ?


   
  Na Dan Ogega
Huenda klabu ya West Ham ikamsajili kiungo wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain, ambaye ako na umri wa miaka 22 baada ya wanabunduki kuamua kumuuza mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Uingereza
Barcelona wanataka kumuuza mbrazil Neymar Santos Jr mwishoni wa msimu huu kwa sababu ya matakwa ya mchezaji huyo huenda yakafilisisha klabu hiyo. Majarida ya Uingereza yanasema kuwa huenda mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya ligi kuu Brazil Santos akahamia Manchester United ambao wako tayari kumpa mkataba wa pauni elfu 300 kwa wiki.
Manchester United huenda wakamsajili mshambulizi wa klabu ya Olympique Lyonnais Alexandre Lacazette, ambaye alikaribia kujiunga na Newcastle kwa kima cha pauni milioni 22 msimu uliopita.
Meneja wa Manchester United mholanzi Louis van Gaal anaamini kuwa ushindi wa kombe la FA msimu huu unaweza kuwa kichocheo cha ufanisi mkubwa kwa klabu hiyo siku zijazo
Meneja wa klabu ya Newcastle mhispania Rafael Benitez huenda akasalia na klabu hiyo hata kama watashushwa daraja baada ya kuzindua miradi ya muda mrefu ya kuiboresha klabu hiyo.
Huenda tineja wa Chelsea Dominic Solanke akagura klabu hiyo baada ya kukataa kutia saini kandarasi mpya. Kandarasi yake inafika kikomo msimu huu huku Chelsea wakipanga kuziba pengo hilo na straika wa klabu ya Fulham Moussa Dembele
Mkurugenzi mkuu wa klabu ya Tottenham Daniel Levy anakabiliwa na wakati mgumu huku wachezaji wengi wa klabu hiyo wakitarajiwa kuitisha nyongeza ya mishahara ikiwa watamaliza miongoni mwa timu nne bora msimu huu.
Mkufunzi wa muda wa klabu ya Aston Villa Eric Black ameweka bayana kuwa hatakubali mkataba wa kudumu wa kufunza klabu hiyo ambayo tayari imeshushwa daraja.
Mnejea anayeondoka wa klbu ya Man City Manuel Pellegrini ameukashifu usimamizi wa klabu hiyo kwa kuatangaza mjo wa Pep Guardiola huku aksema kuwa hatua hiyo iliwaadhiri wachezaji wake jambo lililopelekea kushuka kwa hali yao ya mchezo.
Mwalimu wa Tottenham Mauricio Pochettino amwewakataza wachezaji wake kuhudhuria dhifa ya kuteua wachezaji wa msimuu katika vitengo kadhaa ili kuwaepusha na uchovu kabla ya pambano lao dhid ya Westbrom Jumatatu.
Share on Google Plus

Kuhusu Unknown

Michezo Kenya Tunapenda Spoti

0 comments:

Post a Comment