Ushindi Mmoja Tu!




 
   Na Edwin Mwangi
Baada ya Tottenham Spurs kuvaana sare ya 1-1 na West Brom hio Monday usiku sasa ni dhahiri kuwa Leicester City wameongoza na alama saba huku zikibakia mechi tatu pekee . Hii inamaana kuwa wakiwachapa Manchester United hio Jumapili au wakabane koo ya sare ,pia nao Tottenham wakitereza tu kidogo dhidi ya Chelsea ,pia wako ndani. Kumbuka pia kama Tottenham watavaana sare na Chelsea basi watakuwa na alama 70 na kama vijana wa Raneri watawakamata nunge Mashetani Wekundu basi watakuwa na alama 78 huku zikibakia tu mechi mbili pekee.

Je ,Chelsea watawachapia Liecester City mahasimu wao wa jadi wa mji wa London, Spurs? Ni hio jumatatu siku ya wafanyikazi nchini basi watapanda gari ndege kutembea kulewa kukesha na kutabasamu kwa msimu wenye mavuno mema. Kumbuka mwishoni mwa wiki iliopita kiungo matata wa liecester muhrez alishinda taji la mchezaji bora wa mwaka katika shindano la PFA.
Share on Google Plus

Kuhusu Unknown

Michezo Kenya Tunapenda Spoti

0 comments:

Post a Comment