
Nyota wa klabu ya Montreal Impact ya ligi kuu Canada Didier Drogba. Ametuhumiwa kupunja pesa za msaada
Na Dan Ogega
Mchezaji zamani wa Chelsea na timu ya taifa ya Kodivaa Didier Drogba amekubali kuchunguzwa kuhusu matumizi ya pesa za msaada za wakfu wake wa 'Didier Dogba Foundation'
Kulingana na chapisho la jarida la Daily Mail nchini Uingereza ni pauni elfu 14,115 kati ya takriban pauni milioni 1.7 zilizochangishwa kwa wakfu huo zilitumika kusaidia jamii masikini nchini Kodivaa.
Kwa sasa tume ya kusaidia jamii nchini Uingereza imeanzisha uchunguzi kuhusu matumizi ya pesa hizo huku Drogba akisema kuwa pesa hizo zitatumika ipaswavyo na kwa wakati mwafaka. Kwenye makala katika jarida hilo, imetuhumiwa kuwa takriban pauni elfu 439,321 zilitumika kuandaa dhifa za kifahari zilizohudhuriwa na mabwanyenye na watu tajika duniani huku zingine zikisalia katika akaunti za benki.
Akizungumza na vyombo vya habari akiwa mjini Montreal, Canada, anakochezea klabu ya Montreal Impact Drogba alihoji kuwa miradi yote imefadhiliwa na kandarasi zake za ufadhili huku akikana madai kuwa imefadhiliwa na wafadhili kutoka Uingereza.
"Nina jukumu la kuhakikisha matumizi mazuri kwa pesa hizi. Sitazitumia visivyo kinyume na mipangilio yangu.''
"Nina miradi ya muda mrefu na ninajua chenye nataka kukifanya."
Wakfu huo uliozinduliwa mnamo mwaka 2007, unatekelezwa nchini Kodivaa lakini umesajiliwa nchini uingereza.
Katika kauli ya mapema Drogba aliyesaidia Chelsea kunyakuwa kombe la Ulaya kwa vilabu mnamo mwaka 2012 alisema kuwa alitumia pauni milioni 2.9 katika miradi kadhaa nchini mwake ikiwemo ujenzi wa zahanati na pia katika nyumba za mayatima.
Aitha Drogba amesema kuwa atachukua hatua za kisheria dhidi ya jarida hilo huku akiongeza kuwa litajukumizwa kuwajibikia kila neno katika chapisha hilo.
drogba awajibiki vitendo vyake na ikiwa ni oungo daily mail washtakiwe
ReplyDelete