Welbeck amemfanya Walcott Kuhama Arsenali
Na Dan Ogega
Huenda winga machachari wa Arsenali Theo Walcott akagura klabu hiyo katika soko la majira ya joto baada ya nafasi yake katika kikosi cha kwanza kuwa nadra. Tangu mwezi Januari Muingereza huyo meanza mara moja tu katika kikosi cha kocha mfaransa Arsene Wenger.
Walcott ambaye kwa sasa yuko na umri
wa miaka 27 amefunga mara tano katika
michuano 15 aliyoanza lakini kwa sasa anaketisha benchi huku muingereza
mwenzake Danny Mensah Welbeck na kinda mnaijeria Alex Iwobi wakianzishwa kila
mara
Pia uwezekano wake kuunda kikosi cha
timu ya taifa ya uingereza kitakachoshiriki michuano ya taifa bingwa barani
ulaya mwaka huu imekumbwa ta sintofahamu baada ya meneja wa timu hiyo Roy
Houghson kusema kuwa itabidi atie bidii zaidi.
Kaimu meneja wa zamani wa klabu ya Chelsea
Ray Wilkins anahisi kuwa atahitajika kugura washikabunduki hao wa London ili
kuendelea kuchezea Uingereza.
"Mambo sio mazuri kwa Walcott ikiwa ataendelea kulikamua benchi la klabu ya
Arsenali katika kiwango hiki katika taaluma yake. Kwa sasa anahitajika kucheza
kila mara.
"Kwa sasa yuko kweye mtanziko
kwa sabau hataweza kuinga kama mshambulizi wa kwanza katia klabu yake . Kama
anataka kucheza kama straika basi mstakabali waake haupo klabuni arsenali."
Walcott alijiunga na Arsenali mnamo
mwaka 2006 akitokea klabu ya Southampton.
0 comments:
Post a Comment