Nyota wa Chelsea Eden Hazard awaonea kijicho Tottenham
Na Edwin Mwangi
Kiungo wa kati wa Chelsea Eden
Hazard amesema kwamba yeye na wachezaji
wenzake hawaitakii Tottenham kushinda ligi kuu Uingereza. Spurs wako
alama nane chini ya Leicester huku zikibakia tu mechi nne pekee.
Chelsea ambao ni mabingwa watetezi wanachuana na mahasimu wao wa jadi wa jiji la
London Spur nyumbani tarehe 2 mwezi ujao
na kisha kufunga virago na kisha kupungia mkono kikombe mkono wakicheza na Leicester
15 May, mechi ya mwisho ya msimu huu.
" Mashabiki, klabu na wachezaji
hatutaki Tottenham washinde ligi, " Hazard, 25, alinukuliwa na BBC
"Tunawatakia Leicester kila la heri kwa sababu
wanastahili kuwa mabingwa msimu huu.''
"Tuna mchuano mzuri wiki ijayo
dhidi ya Tottenham na kama tutawashinda basi ni vyema."
Hazard, Mchezaji bora wa 2015, alifunga mara mbili katika mechi kati yao na Bournmouth Jumamosi
wakati Chelsea waliwacharaza Bournmouth4-1 yakiwa ni mabao yake ya
kwanza msimu huu.
Hazard akikabiliana na Spurs
Kiungo wa kati wa Chelsea Cesc Fabregas, zamani akichezea Arsenali kuanzia 2003 hadi 2011, pia anaitakia Leicester ushindi
na anawataka kutwaa ligi kabla ya mechi yao dhidi ya Chelsea.
"Nina imani watakuwa wameibuka
washindi wakati huo," raia huyo wa uhispania alliambia Sky Sports.
"Spurs wanasukuma sana kuhakikisha wamewapiku
Liecester lakini nadhani Liecester watashinda. ”
"Sitaki Spurs washinde na vile
wamefanya msimu huu ningependa Liecester wachukue ligi."


wazi
ReplyDelete