
Na Dan Ogega
Timu ya taifa ya Kenya ya mchezo wa raga kwa wachezaji saba kila upande almaarufu Simba imefuzu fainali ya msururu wa Singapore. Hii ni baada ya kuikwangura Argentina kwa jumla ya alama 15-12 katika mchuano wa nusu fainali uliogaragazwa mapema Jumapili.
Augustine Lugonzo na Frank Wanyama waliifungia Simba ‘tries’ muhimu huku Sammy Oliech akifunga ‘conversion’ moja.
Kigogo Collins Injera alifunga mpira wa adhabu na kufikisha idadi ya alama alizofunga katika misururu yote ya IRB kuwa 1,145 katika mchuano wake wa 335 katika mashindao hayo.
Hapo kabla Kenya iliikalifisha Ufaransa alama 28-07 katika mchuano war obo fainali.
Sasa Kenya itakabiliana na Fiji waliowabwaga wawakilishi wengine wa bara la Afrika Afrika Kusini 26-21.
0 comments:
Post a Comment