Rashford Ndio Dawa Yao



Kinda Marcus Rashford aliisaidia klabu yake ya Manchester United kusajili ushindi finyu wa 1-0 dhidi ya Aston Villa katika uwanja wa nyumbani wa Old Trafford Jumamosi.
Licha ya klabu ya Villa kudhibitisha kushushwa kwa daraja, hawakutisha lango la wapinzani wao hata kidogo. Manchester united walimkaribisha kiranja Wayne Rooney aliyekuwa akirejea kutoa kwa jeraha la muda mrefu huku akidumu kipindi cha kwanza pekee.
Rashford anazidi kuwashangaza wengi baada ya kutumbukiza nyavuni takriban bao saba katika mechi 12 alizochezea mashetani hao wekundu.
Meneja wa klabu hiyo Louis van Gaal amefuahishwa na hali nzuri ya mchezaji huyo huku timu yake ikizidi kusajili ushindi baada ya kufanya vibaya katika michuano ya nyuma. United waliwabwaga Westham 2-1 na kutinga awamu ya nusu fainali ya kombe la FA kati kati ya wiki hali iliyompeleka LVG kuwapumzisha kiungo Michael Carrick na mshambulizi Anthony Martial
Share on Google Plus

Kuhusu Unknown

Michezo Kenya Tunapenda Spoti

0 comments:

Post a Comment