Na Dan Ogega
Mchezaji wa zamani wa klabu ya Liverpool Jamie Carragher anaamini kuwa hatua ya meneja wa Arsenal Arsene Wenger ya kutomsajili straika wa Barcelona Luis Suarez, ndio makosa makubwa zaidi atakayoyajutia katika taaluma yake. Suarez ambaye ni raia wa Uruguay alikuwa ameridhia kuhamia uwanjani Emirates laini mkono ghamu wa Wenger ukamnyima fursa hiyo.
Msimu uliofuata aliisaidia Liverpool
kumaliza katika nafasi ya pili ligini na baadaye akakamilisha uhamisho wa pauni
milioni 75 kwenda Barcelona.
Msimu uliopita alibugia mabao 25 huku
akiwa tayari ashafunga maradufu ya idadi hiyo msimu huu.
Wakati huo huo Arsenal wanazidi
kuchemsha na kusajili matokeo dinu huku mshambuliaji wake mfaransa Olivier
Giroud akiwa mfungaji bora kwa baada ya kucheka na nyavu mara 12 katika ligi
kuu Uingereza msimu huu.
"Ukiangazia miaka 20 ya Arsene
Wenger katika ligi kuu ya premia Uingereza kuna mengi makubwa ambayo
ameyatimiza, lakini mwezi Julai mwaka 2013 hautasahaulika kwa sababu alikosa
kushawishi Liverpool kumuuzia Suarez.’’ Carragher aliandikal katika blogu yake
katika jarida la Daily Mail.
"Wenger ana rekodi ya kuwa
mmakinifu katika matumizi ya pesa kwa sababu yeye hutumia fedha za klabu pale
anapohisi kuwa atapata matokeo mazuri. Hii ni ishara ya uhuru wa kungojea na
ungojea aliopewa na klabu hiyo.’’
‘Msimu uliopita katika majira ya
joto kwa mfano alisajili tu mchezaji mmoja tu ambaye ni golikipa wa Chelsea
Petr Cech na akapuuza kusajili kiungo yeyote.’’
"Kama Arsenal wangeshinikiza
kumsajili, labda kwa toleo la pauni milioni 50 naamini wangenyakua taji la
ubingwa wa ligi kuu Uingereza mara mbili katika misimu mitatu iliyopita. Huo ndio
ukweli kumhusu Suarez kwa sabau timu yoyote aichezeayo, yeye huwa vuruta hadi
upeo wa juu.’’

0 comments:
Post a Comment