Mbona Wakenya Hungara Katika Riadha ?

   

 
   Na Dan Ogega
  Kenya imetamalaki riadha katika siku za nyuma katika vitengo mbali mbali jambo ambalo limepelekea maswali kuibuka kuhusu sababu za ufanisi huo. Michezo Kenya imezama na kuibuka na baadhi ya vichocheo hivyo.
    Katika siku za nyuma wanariadha kutoka kenya walikuwa wamebanwa kushiriki mashindano ya kimataifa jambo lililopelekea matokeo duni kwa bara ka Afrika. Pindi tu vikwazo hivyo vilipoondolewa kenya ilianza kutia fora siku baada ya siku. Miundo msingi ya michezo na pia ufadhili kutoka kwa kampuni za kimataifa kama vile Nike, Adidas, IAAF vimechochea pakubwa ufanisi katika matokeo kwa taifa hili katika ulingo wa kimataifa. Pia mjo wa mameneja wa kigeni kumesababisha kuimarika kwa viwango vya riadha nchini.

Baadhi ya sababu hizo ni:
 
Kuchuma Riziki


  Baadhi ya wanariadha wanavutiwa na kipato kinachoandamana na ushindi katika mbio mbali mbali. kinyume na bara ulaya ambapo vipaji hutunzwa tangi utotoni. Chipukizi wengi wako na uwezo wa kuhudhuria shule huku wakikuza talanta yao. Pia ufadhili kutoka kwa vyuo vya kigeni huchochea bidii ili waweze kujishindia nafasi za kuendeleza masomo yao katika mataifa ya kigeni.

  Motisha 

bara la afrika linakumbwa na changamoto lukuki kila uchao. nafasi  ya chipukizi kujinyakulia ufadhili, kandarasi za matangazo na pia pesa ni kichocheo kikubwa kwa ufanisi unaoshuhudiwa kwa wanariadha wa kenya katika ulingo wa kimataifa.

 Jeni za ushindi 

   Wanariadha wakenya wana jeni za kustahimili kufanya mazoezi na kukimbia kwa muda mrefu. Uwepo wa jeni aina ya ACTN-3 katika chembechembe za damu huchangia kudumu kukimbia kwa muda mrefu. Pia misuli yao inaweza kustahimili kazi kwa muda mrefu. Seli za miili yao huweza kuzalisha chembechembe za aina ya mitochondria ambazo huifadhi hewa safi ya oksijeni jambo linalowafaidi na pumzi ya ziada kwa muda mrefu

Misuli Mikakamavu

Misuli ya wanariadha wakenya inaweza kuwaepusha kuchoka haraka ambazo huweza kustahimili viwango vya chini vya hewa safi ya oksijeni na pia zina idadi kubawa ya seli za mitochondria ambazo huzalisha nishati.

 Mazingira ya Nyanda za Juu

Asilimia kubwa ya wanariadha wakenya hutoka katika eneo la bonde la ufa ambalo linapatikana kwa muinuko wa takriban mita


Share on Google Plus

Kuhusu Unknown

Michezo Kenya Tunapenda Spoti

0 comments:

Post a Comment