Na Dan Ogega
Ushindi katika
kome la FA hautakiokoa chuma cha Louis van Gaal kwani atafurushwa mwishoni mwa
msimu huu. Haya ni kulingana na kauli ya mwanahabari wa jarida la The Sun Neil Custis ambaye pia
anahisi kuwa huendaJose Mourinho akaridhi cheo cha mholanzi huyo katika uwanja
wa Old Trafford.
Ushindi wa 2-1 dhidi ya Everton siku
ya Jumamosi unamaanisha kuwa sasa mashetani hao wekundu wana nafasi ya kukata kiu
ya taji ambayo imedumu tangu mwaka 2013. Mkataba wa Van Gaal ambaye amekosolewa
sana katika siku za hivi karibuni baada ya matokeo ya kuvunja moyo unatamatika
mwaka huu huku Curtis akihoji kuwa uamuzi wa kumtimua tayari ushafanyika.
"Nina uhakika kuwa uamuzi
ushafanyika kuwa Mourinho atawasili Manchester United msimu ujao.
"Mourinho amenawiri kila mahali
ameenda jambo ambalo ni tiketi yake kumrithi van Gaal.
"Sidhani kuwa ushindi dhidi ya
Everto utafuta rekodi yake mbaya kwa muda wa miezi 18 iliyopita ambayo kiukweli
ni mbovu sana.
"Kama tungeshuhudia matokeo
kama ya jana kwa muda huo basi hatungedhubutu kuuliza kuhusu umilisi wake
kufunza United.’’
Licha ya shinikizo la kuleta ufanisi
kwa klabu hiyo van Gaal amepewa heko kwa kuwaleta chipukizi katika kikosi chake
jambo ambalo limemwauni japo kwa kiduchu. Lakini Curtis anahoji kuwa jambo hilo
lilichangiwa na wachezaji wa kikosi cha kwanza kuwa majeruhi.
"Kuhusu suala la kuwaleta vijana katika
kikosi cha kwanza kwangu sio mshangao kwa sababu ya hali ya majeraha. Lisingejiri
hatungepata nafasi ya kuwaona kina Marcus Rashford.
"Labda mara moja kwa kila mwezi
tuna wakati tunaposema, labda kuna kitu kizuri kinakuja kuna ishara ya
maendeleo.’’
"Kwa vyovyote vile chochote
kitakachojiri tangu sasa hadi mwisho wa msimu hakitabadili mustakabali wa Van Gaal
."
Jose Mourinho yuko huru kujiunga na
United kufuatia kutimuliwa kwake kutoka Chelsea mnamo mwezi Disemba mwaka jana,
United walimaliza katika nafasi ya
nne msimu uliopita lakini wakabanduliwa kutoka mechi za klabu bingwa barani Ulaya
na pia kwenye kombe la Europa League na mahasimu wa jadi Liverpool katika awamu
ya 16 bora.

0 comments:
Post a Comment