Chelsea wachemsha
nyumbani
Na Edwin Mwangi
Mchezaji wa zamani wa klabu ya Liverpool Graeme Souness amemkashifu kiranja wa Chelsea John Terry kwa kichapo cha Jumamosi dhidi wa Man City ugani Stanford Bridge . Souness anahoji kuwa kuwepo kwa Terry kungezuia kichapo cha 3-0 machoni mwa mashabiki wao wa nyumbani. Mchezaji na straika matata wa City Sergio Aguero alidhihirisha umahiri wake kwa kutia wavuni mara tatu na kudidimiza na kuchafua mchezo wa Chelsea wa kitabu na kumwaacha mkufunzi wa muda Guus Hiddink kuandikisha kichapo chake cha kwanza nyumbani.
Chelsea walianza mchuano huo kwa
kishindo na kutia matumaini mashabiki lakini uwepo wa mchezaji wa zamani wa Wolfsburg
Kevin De Bryune kuhemesha timu yake ya zamani na kuwaadhibu
mabeki na mbio zake za kanga.

0 comments:
Post a Comment