Mashabiki
wengi wa klabu ya Man United wangependa sana msimu huu ukamilike haraka iwezekanavyo kwa sababu ya masaibu kibao klabu hiyo imeshuhudia kwa mwaka mmoja uliopita. Meneja wake mholanzi Luis van Gaal alitarajiwa kuwa na ufanisi mkubwa baada ya kutumia zaidi ya pauni milioni 250 kuimarisha kikosi chake lakini matokeo yamekuwa kinyume. Labda kuondoka kwa wachezaji muhimu kama Luis Nani , Robin van Persie, Rafael da Silva na Anderson Oliveira ndio chanzo cha kitumbua cha mashetani hao kuchemsha katika kila kikombe wlichokuwa waking'ang'ania.
Licha ya masaibu hayo kumekwa na sababu kadhaa za kuwa na matumaini katika siku za usoni. Mojawepo ya sababu hizo ni mjo wake kinda Marcus Rashford ambaye ameshangaza wengi kwa umahiri wake katika ufungaji mabao. Dogo wengine ambao wana uwezo wa kuleta mabadiliko katika himaya ya Old Trafford ni pamoja na kiungo mshambulizi Andreas Hugo Hoelgebaum Pereira, Jesse Ellis Lingard, Donald Love na Cameron Jake Borthwick-Jackson ambao wameonyesha umakinifu mkubwa katika uchezaji wao licha ya kuwa na umri mdogo.
Safu ya ushambulizi bila shaka ndio imekumbwa na mchecheto mkubwa ikizingatiwa kuwa klabu imefanikiwa kutumbukiza mabao 69 tu msimu huu ikiwa na idadi ndogo zaidi kwa klabu hiyo katika msimu mmoja.
Nahodha wa mashetani wekundu Wayne Mark Rooney anaongoza katika chati za wafungaji bora baada ya kucheka na nyavu mara 14 ikiwemo 'hat-trick' moja na ' brace' moja. Mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa aliyejiunga na klabu hiyo akitokea AC Monaco Anthony Martial anamfuata kwa karibu akiwa na magoli 13.
Takwimu kamili ni kama ifuatavyo
| Mchezaji | EL | FA | LG | LC | Jumla | ||
|---|---|---|---|---|---|---|---|
| 1 | Wayne Rooney | 1 | 0 | 2 | 7 | 1 | 14 |
| 2 | Anthony Martial | 2 | 1 | 1 | 8 | 1 | 13 |
| 3 | Juan Mata | 1 | 0 | 2 | 5 | 0 | 8 |
| 4 | Memphis Depay | 1 | 2 | 0 | 2 | 0 | 7 |
| 4 | Marcus Rashford | 0 | 2 | 1 | 4 | 0 | 7 |
| 5 | Ander Herrera | 0 | 1 | 0 | 3 | 0 | 5 |
| 5 | Jesse Lingard | 0 | 0 | 1 | 4 | 0 | 5 |
| 6 | Marouane Fellaini | 0 | 0 | 1 | 1 | 0 | 3 |
| 7 | Daley Blind | 0 | 0 | 1 | 1 | 0 | 2 |
| 7 | Chris Smalling | 1 | 0 | 1 | 0 | 0 | 2 |
| 8 | Adnan Januzaj | 0 | 0 | 0 | 1 | 0 | 1 |
| 8 | Andreas Pereira | 0 | 0 | 0 | 0 | 1 | 1 |
| 8 | Morgan Schneiderlin | 0 | 0 | 0 | 1 | 0 | 1 |
| 8 | Bastian Schweinsteiger | 0 | 0 | 0 | 1 | 0 | 1 |

0 comments:
Post a Comment