Hazard bado bora, huku Pogba akimezewa mate na Chelsea
Eden Hazard
Na Edwin Mwangi
Raia wa ubelgiji amestahimili ukame wa mabao ugani Stamford Bridge msimu huu , hata baada ya kushinda taji la PFA msimu uliopita.
RiyadMahrez wa Leicester alinyakua taji hilo lakini meneja Hiddink amemkababithi upeo Hazard kutetea uwezo wake msimu ujao
‘Akiwa na hali njema ya afya na mchezo ni mchezaji
bora zaidi” alinena Hiddink .
"Amekuwa na simu mbaya na ni vigumu kwa mchezaji mwenye taathima kama yake.
."Amekuwa akiumia na ni vyema tumpatie matibabu na kumtayarisha kureje kwa kishindo msimu ujao.’’
Katika dirisha la uuzaji na ununuzi wa wachezaji meneja wa klabu ya, Juventus Giuseppe Marotta amekuwa akifanya mazungumzo na kuweka mikakati ambayo kwa namna Fulani inaweza kuadhiri mipango ya Chelsea.
Paul Pogba
Chelsea wamekuwa wakimmezea mate kiungo wa kati wa Juventus Paul Pogba huku mshambuliaji Paulo Dybala akiwa nyavuni zao.
Juve wako tayari kumweka mchezaji Juan Cuadrado wa mkopo kama mchezaji wa kudumu ikiwa wanasamawati hao wataonesha nia ya kumwinda nyota huyo mfaransa.
Kwa sasa anakadiriwa kugharimu kitita cha pauni milioni 78 na alipendekezwa na meneja mtarajiwa wa Chelsea Antonio Conte akiwa Juve.
Juan CuadradoConte mwenye umri wa miaka46, anaweza kumshawishi Pogba au Dybala lakini Marotta ameshikilia kuwa hili halitafanyika.
“Pogba na Dybala ni miamba wa timu , kwa hivyo hatuwezi wauza," Marotta alisema kwa mujibu wa Mediaset Premium.
Mkolombia Cuadrado atarejea Chelsea mwishoni mwa msimu huu.
0 comments:
Post a Comment