Na Dan Ogega
Dhana ambayo imeghubika washikadau wa klabu ya Man city ni kuwa
wanahitaji kufuzu kwa awamu ya nusu fainali ya kombe la klabu bingwa bara ulaya
mara nne au zaidi ndiposa wapate kulinyakua. Hii ni kwa sababu awanu ya maondoano ni karata ya bahati nasibu na
hakuna kutegemea majanga ya ghafla kwa klabu kubwa zinazoshiriki dimba hilo.
Mashabiki wa klabu hiyo walifurahia
habari kuwa huenda Cristiano Ronaldo hangeshiriki mchuano wa mkumbo wa kwanza
hii leo kiwarani Etihad, lakini iwapo atakuwa fiti kucheza basi itabidi
wamkabili vilivyo kama wanataka kucheza mechi ya marudiano ugani Santiago
Bernabeau mwezi kesho wakiwa na matumaini.
Licha ya zimwi hili linaloikabili
Man City ni muhimu kukumbuka kuwa Kamari hii inaweza kugeuza kibao kwa madrid
ikiwa wakakosa kuwa katika ubora wao kimchezo. Los Blancos walitinga nusu
fainali lca kumfukuza Benitez jambo lililosambaratisha maazimio ya klabu hiyo.
Aliyeridhi mikoba yake mfaransa
Zinadine Zidane akizungumza na wanahabari jana alidhihirisha kuwa kuna
ushikamano fulani licha ya kuwepo mushkeli kidogo kikosini.
Mfaransa huyo huleta mchecheto na
kuzoa matokeo mazuri. Tangu enzi za kufunza kikosi cha pili cha Madrid yaani
Castilla Zidane alikuwa amezoea uhuru wa
kufanya kazi kwa ushirikiano kutoka kwa kila mshikadau. Kikosi kilikuwa
kikisafiri kwa basin a pia alikuwa amepewa hela za kusajili wachezaji jambo
ambalo ni msamiati kwa meneja wa sasa wa Castilla Luis Miguel Ramos.
Hadi sasa ni bayana kuwa rais wa
klabu hiyo Florentino Perez anaamini kuwa Zidane anaweza kuongoza klabu hiyo
katika harakati za kufikia upeo mpya, nafasi ambayo imekuwa kama kucheza na
shilingi kariku na tundu la msalani. Mameneja kadhaa wamefurushwa akiwemo Jose
Mourinho, Carlo Ancelotti na Manuel Pellegrini. Msimu uliopita alimpuuza wakati
wa akimnyakuwa Rafa kutoka Napoli huku Zizou akionekana kutoridhishwa na uamuzi
huo.
Kwa hivyo hatua ya kujaza pengo la
Benitez na Zizou ni uamuzi ambao haukutarajiwa na wengi na ambao haukutarajiwa
kuleta mafanikio kaltika klabu hiyo.
Ramos anaripotiwa kutoridhika na maamuzi ya uongozi wa Real Madrid
Nyuma ya pazia la kuuza sera za klabu
katika mahojiano ya jana jioni, kuna ulegevu fulani ambao unaonekana katika
kikosi chake. Katika michuano mikubwa sampuli ya huu wa leo nyota wao CR7
hutarajia viungo wenzake kama James Rodriquez na Marcelo Vieira kumpitishia
mpira na ikiwa watakosa basi yeye hubaki akiteta.
Kila wakati mchezaji ghali Zaidi
Gareth Bale hujipata ako pembeni mwa uwanja hii ikiwa ni baada ya lalama za
Ronaldo baada ya Bale kujaribiwa kama straika.
“Mbona mnamchezesha hapa? Hii ni nafasi yangu.’’
Alibweka CR7
Ronaldo akilalamikia hali duni ya wachezaji wenzake uwanjani
Hali ya kujipendelea inaweza
kuchipuka katika mazingira sampuli hii.
Msimu uliopita kiranja wa klabu hiyo Sergio Ramos aliitisha kura ya maoni ya
ikiwa wangemuondoa daktari wa klabu hiyo baada yake kushukiwa kuwadukua
wachezaji katika vyumba vya kubadilisha mavazi.
Ni kikosi kinachosheheni wachezaji
wanaopigania umaarufu huku Ramos akiwa mmoja wao. Jambo linaloharibu mambo
zaidi ni kuwa alitamani kugura klabu hiyo miezi minane iliyopita. Uhusiano kati
yake na Perez ni mgumu kwa wakati huu huku Ramos akidhibitisha kuwa alikuwa
amekubali makataa ya kuhamia Manchester United. Alibaki tu ili kuendeleza sera
za Perez ambaye ni kero kwa wafuasi wa klabu hiyo.
Ramos pia alisazwa ili kupiga jeki
idadi wa wahispania wanaounga kikosi cha kwanza cha klabu hiyo. Kwa maana hiyo,
alimkabidhi Ramos mkataba wa kima cha pauni milioni 10 na kuzima uhamisho wa
Nicolas Otemendi aliyejiunga na City.
Kudhibiti mienendo ya wachezaji
wakubwa sio kazi rahisi. Kiujumla ni kuwa muitaliano Ancelotti alijaribu
kutekeleza wajibu huu. Labda ni kwa sababu aliwapa uhuru wa kucheza bila
shinikizo.
Hali hii ya mshikemshike huenda
ikanufaisha City kwani wakitilia maanani vigezo vya uchezaji bora huenda
wakawapiku Real usiku wa leo.





0 comments:
Post a Comment